Ibrahim Class apanda ubora

BONDIA wa ngumi za kulipwa Ibrahim Class amepanda katika ubora baada ya kufikisha nyota nne kutoka tatu na nusu aliyokuwa nayo kwa muda mrefu.
-
Class aliweka taarifa hizo kwenye mtandao wake na kusema kuwa Mwenyezi Mungu, bidii, sapoti ya familia, mashabiki na timu yake vimemuwezesha kufikia hatua hiyo.
-
“Hii ni heshima kubwa na motisha ya kuendelea kupambana zaidi bila
kuchoka,”amesema na kuongeza kuwa safari bado inaendelea na lengo ni kufika juu zaidi.
-
Spotileo ilimtafuta kuzungumzia ubora huo na yeye kusema kuwa imetokana na mapambano mazito aliyocheza mwaka jana na mabondia tofauti wa viwango vya juu.
Takwimu za mtandao wa ngumi wa boxrec zinaonesha Class anashika nafasi ya kwanza Tanzania kati ya mabondia 90 wa uzito wa Super feather na nafasi ya 32 duniani kati ya mabondia 1,954.
-
Miaka miwili iliyopita hajapoteza pambano lolote liwe la ndani au la kimataifa.