Maxi Nzengeli awatoa presha Wanayanga, afikiria mechi ya Kagera Sugar Jmosi


"Mimi sihusiki na tetesi,tetesi ni zenu nyie ili muuze habari.

Mimi nafanya kazi yangu kama mwajiriwa wa Yanga.
Kama niko hapa Yanga kwa mkopo mimi silijui hilo na wala sitaki kujua nilinunuliwa pia sijui.

Lakini na nyie muwe mnajihoji Mwenzangu Mayele walisema hivyohivyo kuwa yupo kwa Mkopo lakini alicheza miaka 2 na kuuzwa na Yanga kwenda Pyramid.

Kitu kikubwa ninachokiwaza je kocha atanipa nafasi Jumamosi niweze kuitetea nembo ya mwajiri wangu Yanga? Niulize hilo swali.

Maxi Nzengeli mchezaji wa Yanga anayemezewa mate na Timu kibao Tanzania na Afrika Kusini.