Chippa United yamtema Majogoro

Kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania Baraka Majogoro ameachana na klabu yake ya Chippa United kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Majogoro (27) ambaye alijiunga na miamba hiyo ya Afrika Kusini mnamo Agosti 2023 akitokea KMC Majogoro amekosa mechi tano tu kwenye michuano yote klabuni hapo msimu huu.

Nyota huyo wa zamani Ndanda Fc, Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar kwa sasa ni mchezaji huru na upo uwezekano wa kuendelea kukipiga Afrika Kusini huku vilabu kadhaa vikitajwa kuhitaji saini yake.