1998 Yanga waliazima jezi za Taifa Stars


Mwaka 1998 Yanga walicheza hatua ya robo fainali ya CACL kwa mara ya kwanza dhidi ya Asec Mimosa ya Ivory Coast.

Lakini cha kuvutia zaidi katika mchezo huo ni Yanga walipoazimwa jezi za timu ya taifa (Taifa stars) ili wazitumie katika mchezo huo,lakini pia waliazima wachezaji kutoka Simba ili wawasaidie na pamoja na msada huo bado Yanga alifungw bao 3 kwa 0 katika dimba la uhuru.

Wachezaji walioazimwa toka Simba ni Monja liseki na Shaaban Ramadhani.

Yanga waliazima jezi za Stars sababu walikua na jezi za njano tu ambazo zilifanana rangi na jezi za Asec.