Sikutamani kuichezea Yanga - Sureboy
Salum Abubakar ( Sure Boy) miongoni mwa mahojiano yake aliyowahi kufanya na AzamTV Alisema hivi
“ Mimi ni mshabiki wa yanga toka nikiwa mtoto nimekua katika familia ambayo wanapenda yanga kwahiyo hata
Mimi nilikuwa napenda Yanga , sikutamani kucheza Yanga hapa awali kwasababu nilikuwa najua nitaumia alafu mashabiki wataumia sana ,
Yanga timu yenye mashabiki wengi ambao wanapenda sana timu yao ”,
Kwanini nimeandika nukuu hii ? Vijana wengi wanaocheza soka wanandoto za kucheza Simba na Yanga lakini hawajui njia nzuri ya wao kufika hapo, fikiria kama sure boy angetaka kwenye yanga toka muda kipindi kile umri na energy ni nyingi ingekuwaje angeshindwa ?
Vijana katika soka waambie wawe na uvumilivu na sehemu walizopo mafanikio katika soka hayataki haraka. mara kadha ambazo sure boy anapata nafasi katika Kikosi cha Yanga kwasasa bado Kiwango chake kinatoa majibu kwa vijana kuwa unatakiwa kuheshimu mpira na kuishi katika misingi ya soka.
1 : Utulivu mkubwa Mali inapokuwa mguuni
2 : Pasi elekezi Kwa usahihi mkubwa
3 : Kutoathilika na kukaa nje Kwa muda mrefu
4 : Kukubali Kuwa Kuna muda wa Kucheza upo kwani awali alicheza sababu muda ulifika.