Kaizer Chief kumng' oa Tshabalala Simba

Kocha Mkuu wa klabu ya Kaizer Chiefs Nasreddine Nabi, imedaiwa kuwa anatafuta Beki wa kushoto na tayari amelipendekeza jina la Beki wa klabu ya Simba Mohamed Hussein kwenye uongozi wa klabu hiyo.

Nabi amewasisitiza mabosi wa klabu hiyo kuwa atafurahi kama ataletewa Tshabalala kutokana na ukweli anaujua uwezo wake, Kwani Lengo lake ni kuona upande wa kushoto wa ukuta wa Timu hiyo unaimarishwa zaidi.

Mkataba wa Tshabalala na Simba utamalizika mwishoni mwa msimu huu na Kaizer inapiga hesabu kama itamkosa kwa sasa basi itasubiri beki huyo hadi mwisho wa msimu ili impate kiulaini.

Katika msimu huu beki huyo amecheza mechi zote za kimataifa na kufunga bao moja, huku katika Ligi Kuu Bara akifunga bao moja na kuasisti mara tatu.