Aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Mmiliki wa Shule za Alliance (Alliance Schools), James Marwa Bwire amefariki Dunia usiku wa Januari 25 akiwa jijini Mwanza baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Ukurasa rasmi wa Instagram wa klabu ya Alliance Football Club umethibitisha kifo cha Bwire ambaye ni muasisi wa Alliance School Sports Academy, ambayo inamiliki timu mbili za Alliance Girls inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) na Alliance Football Club inayoshiriki First League.
Alliance Academy imeibua vipaji vya wacheza soka wengi wa kiume na wa kike kama Aisha Masaka anayekipiga katika Ligi Kuu ya Wanawake England akiwa na timu ya Brighton.
Aisha Mnunka anayekipiga Simba Queens, Israel Patrick Mwenda anayekipiga Yanga, Hance Masoud Msonga ambaye yupo KMC na wengine wengi.