Baada ya kupokea ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali, klabu ya Yanga imelegeza msimamo na sasa huenda ikamuuza mshambuliaji Clement Mzize katika dirisha lijalo la usajili, imefahamika
Wakati klabu nne za Uarabuni zikisubiri majibu ya Yanga juu ya utayari wao wakiwa tayari wameshaweka fedha ndefu mezani, taarifa mpya ni kwamba kuna klabu nyingine ya Ulaya nayo imepiga hodi ikimtaka mshambuliaji huyo.
Ukiacha ofa za klabu hizo kutoka Afrika Kaskazini zinazofikia Sh2 Bilioni, klabu hiyo ya Ubelgiji inataka kutoa zaidi ya fedha hizo kufikia 2.5 bilioni.
Mmoja wa maafisa waandamizi wa Yanga amedokeza uwezekano wa Mzize kuuzwa baada ya klabu kuvutiwa dau hilo lakini muhimu zaidi ni kuzingatia maslahi ya mchezaji
“Tunafikiria kufanya biashara fedha zinazosemwa ni nyingi unajua pia tunataka kufikiria juu ya maisha ya baadaye ya mchezaji ili akajiendeleze tutaangalia ofa ipi itakuwa sahihi zaidi kwa klabu na kwake,” Afisa huyo alinukuliwa na Mwanaspoti
Msimu huu Mzize yuko ‘on-fire’ akifunga mabao 12 katika mashindano yote pia akitoa assist nne
Amefunga mabao 5 katika ligi ya mabingwa kuanzia hatua ya awali huku akifunga mabao 6 katika ligi kuu, bao 1 akifunga kwenye Ngao ya Jamii