Timu ya Simba SC jioni ya leo imewajibu watani zao Yanga, baada ya kuilaza Kilimanjaro Worries ya Kilimanjaro mabao 6-0 mchezo wa mtoano kombe la CRDB uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Valentino Mashaka katika dakika ya kwanza aliifungia Simba kabla ya Ladack Chasambi dakika ya tatu kufunga la pili na Patrick Sebastian dakika ya nane alijifunga.
Dakika ya 21 Joshua Mutale leo aliweza bao na Steven Mukwala dakika ya 48 akifunga bao la tano kabla ya Edwin Balua dakika ya 79 kufunga bao la sita