Aziz Ki awaaga Wanayanga

Mfungaji Bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu bara ya NBC Primier League na timu ya Yanga SC Stephanie Aziz Ki ameanza kuwaaga mashabiki wa timu hiyo na akidai kwamba hatoendelea kusalia kwenye ardhi ya Tanzania.

Uongozi wa Yanga chini ya Rais wake Injinia Hersi Said alitangaza kuwauza Aziz Ki na Clement Mzize na kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kwamba nyota hao wawili wameuzwa.

Aziz Ki na Mzize inasemekana watajiunga na Klabu ya Al Itrihad ya Libya na ikiwapa Yanga mabilioni ya shilingi.

Aziz Ki anatumia muda huo kuwaaga mashabiki wa Yanga ambao amekaa nao vizuri na kuweza kuwaletea mafanikio kadhaa na yeye akishinda tuzo ya mfungaji Bora na mchezaji Bora (MVP) wa Ligi hiyo