Tumezoea kutoa bonus kwa wachezaji wetu- Mwagala

Msemaji wa Tabora United Christina Mwagala amemshangaa Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally kuhusu wachezaji wa Tabora United kupewa bonus ya shilingi milioni 50 endapo wataifunga Simba Jpili.

"Mie namshangaa sana Ahmed anakuwa muoga muoga, mtoto wa kiume hutakiwi kuwa muoga nilazima ukabiliane na tatizo ambalo utakutana nalo.

Inshu ya Bonus ndio naona watu wanaikuza kuza ila sisi bonus tumeanza kupewa tangu tumeanza Msimu na mkuu wetu wa Mkoa, Timu ikitoa sare ni milioni 5, ikishinda ni milioni 10.

Lakini kuelekea mchezo dhidi ya Simba amewiwa kutuongezea dau la milioni 50, kwahiyo imekuwa kawaida yetu kula na kunywa na mkuu wetu wa Mkoa wa Tabora.'' Christina Mwagala, Afisa habari wa Club ya Tabora United.