Yanga yaitisha Kagera Sugar kwa bao 5-0

Mabingwa watetezi wa kombe la CRDB Benki au maarufu FA Cup, Yanga SC jioni ya leo imeanza vema kampeni yake ya kutetea ubingwa wake baada ya kuilaza Copco ya Mwanza mabao 5-0 uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao wakitoka kuondoshwa katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika wiki iliyopita, wakipata bao la kwanza kupitia Shekhan Khamisi dakika ya 35, Prince Dube dakika ya 57 aliifungia Yanga bao la pili.

Lakini dakika ya 67 Maxi Nzengeli alipachika bao la tatu kabla ya Duke Abuye dakika ya 77 kufunga bao la nne, na Mudathir Yahya dakika ya 84 kufunga idadi ya mabao kwa kuandika bao la nne.

Kesho watani zao Simba watacheza na Kilimanjaro Worries katika uwanja huo huo kuwania kombe hilo la FA