Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Yanga wamepata tiba fasta


BAADA tu ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, vigogo wa Yanga waliitana haraka na kufanya tathmini ya kile ambacho kimewakwamisha na kupitia kikao hicho yapo waliyoyabaini na kuna maamuzi walichukua, ikiwamo kuigusa kamati ya mashindano ya klabu hiyo.

Kwanza kwa pamoja walikubaliana kwamba timu yao ilistahili kupata ushindi dhidi ya MC Alger ya Algeria katika mechi ya mwisho ya makundi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, wikiendi iliyopita ambayo iliwakwamisha kumaliza nafasi ya pili kwa Kundi A na kuvuka kwenda robo fainali.

Pili waligundua utaratibu wa wachezaji kufanya mazoezi wakitokea nyumbani na kisha kukutana siku chache kabla ya mechi unawapa uhuru uliopitiliza ambao unaleta athari hasi kwa timu.

Kutokana na hilo, klabu hiyo imepanga kufanya mambo mawili ambayo inaamini yatakuwa suluhisho kwa siku za usoni.

Jambo la kwanza ambalo imeamua kulifanya ni kufanya maboresho ya kamati ya mashindano na kuna baadhi ya watu itawapunguza na wengine kuongezwa ili kuipa nguvu zaidi.

"Ni maboresho ya kawaida ambayo yamekuwa yakifanyika mara kadhaa pindi msimu unapomalizika au pale na uongozi unaona kuna sehemu inayumba hivyo wala sio jambo la ajabu au la kushangaza kwa vile lengo ni timu ifanye vizuri," kilisema chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Yanga.

Timu hiyo pia imeamua kurudisha utaratibu wa kambi kwa wachezaji wake ambayo itaanza rasmi leo huko Avic Town Kigamboni.

"Wachezaji wataingia kambini kesho (leo) na itakuwa endelevu tofauti na zamani na walikuwa wakitokea nyumbani na kisha kukutana siku chache kabla ya mechi," kilisema chanzo hicho.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa