Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia anayechezea Yanga iliyoondolewa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika Clatous Chama amefichua kuwa pindi atakapokuwa anaelekea kustaafu soka ndoto zake ni kurudi kuichezea Simba kwa mara nyingine.
“Nikikaribia kustaafu, timu ya kwanza kuipa kipaumbele cha kuichezea ni Simba ila kama wakinikataa ndio ninaweza kwenda timu nyingine kumalizia soka,” alisema Chama.