Tshabalala amkaribisha Chama Msimbazi

Baada ya kiungo mshambuliaji Clatous Chama ambaye kwasasa anaichezea Yanga kudai kwamba atarejea Simba kumalizia soka lake (kustaafu).

Mchezaji mwenzake Mohamed Hussein Tshabalala amemjibu na kumkaribisha Msimbazi lakini wenye timu yao watakapoamua.

Chama aliichezea Simba kwa mafanikio na msimu amejiunga na Yanga lakini hajawa na furaha kutokana na kuwekwa benchi na makocha wote wawili (Gamondi) na (Ramovic) hivyo anatamani kurudi Msimbazi.

"Nimeona hii taarifa kaka kua unahitaji kuja kuitumikia Simba na kustaafu ukiwa Simba sio wazo baya ni wazo zuri ila wenye Simba ni mashabiki wao ndio watatoa maamuzi sahihi", alisema Tshabalala beki wa kushoto wa Simba SC


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI