Morrison kuikosa Yanga Februari 5

Winga mpya wa klabu ya KenGold FC, Bernard Morrison ataikosa michezo ya awali ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu bara ya NBC kutokana na kuwa hajakuwa sawa kucheza uwanjani kutokana na jeraha ambalo alikuwa anajiuguza.

Bernard Morrison alifanyiwa upasuaji wa goti ambao ulimfanya akae nje msimu mzima.

Bernard Morrison ataukosa mchezo kati ya KenGold FC dhidi ya Yanga SC utakaopigwa Februari 05, katika uwanja wa KMC Complex.

Morrison kwasasa anafanya mazoezi maalumu ya pekeake bado hajaanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake.