Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2024

Uongozi wa Yanga kuundwa upya

Picha
Muda wowote kuanzia sasa Uongozi wa klab ya Yanga utatangaza mabadiliko mapya ndani ya Uongozi wa klabu yao, Wapo watakaoenguliwa kutokana na sababu mbali mbali na yapo maingizo mapya yataingia kwenye nafasi zao huku lengo kuu likiwa ni kuboresha zaidi kila nafasi kwenye klabu yao kuwa bora.

Diamond Platnumz azua mshangao mtandaoni

Picha
Picha mpya kutoka kwa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Picha hii imezua gumzo mtandaoni kwani baadhi ya watu wanadai Diamond Platnumz amepata Mwanamke mwingine tofauti na Zuchu huku wengine wakidai kuwa anayeonekana kwenye picha hii ni Zuchu. Ukiangalia vizuri picha hizi, huyo Mwanamke ni Zuchu au siyo Zuchu?

Chama, Aziz Ki wanahitaji kuongezewa ubora

Picha
Kocha mkuu wa Yanga SC Sead Ramovic raia wa Ujerumani amesema wachezaji wake wawili Clatous Chama na Stephanie Aziz Ki ni wazuri ila wanahitaji kuongezewa ubora ama sivyo watapotea. 'Wapinzani wetu walikuwa wagumu nawapongeza,tumepata alama tatu ila bado napaswa kuongeza baadhi ya vitu kama vile fitness na vitu vingine taratibu taratibu. Chama na Aziz wote ni wachezaji wazuri japo napaswa kuwaongezea ubora wao hasa fitness", amesema Ramovic .

Mtibwa Sugar kurejea Ligi Kuu

Picha
Timu ya Mtibwa Sugar wanaendelea kufanya vizuri kwenye ligi ya Championship baada ya kuilaza Mbuni mwbwo 2-0 huku ikiwa imeshinda mchezo wa nane kati ya 11 iliyocheza. Juma Luizio dakika ya 31 alitangulia kuifungia bao la kwanza kabla ya Anuary Jabir dakika ya 69 kufunga bao la pili. TAKWIMU ZA MTIBWA KAMA ZILIVYO 11 Mechi 08 Ushindi 02 Sare 01 Vipigo 19 Magoli ya kufunga 05 Magoli ya kufungwa 07 Clean Sheet Kwasasa iko kileleni .

Yanga yaamkia Ruangwa

Picha
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC usiku huu imeamka usingizini mikononi mwa Namungo FC baada ya kuilaza mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa mkoani Lindi. Kwa ushindi huo sasa Yanga imrfikisha pointi 27 ikiendelea kuifukuza Simba iliyo kileleni kwa tofauti ya alama moja. Kennedy Musonda dakika ya 49 aliwaamsha mashabiki wa Yanga kabla ya Pacome Zouzoua dakika ya 68 kuongeza bao la pili, Namungo FC inayonolewa na Juma Mgunda imeendelea kufanya vibaya na kuhatarisha nafasi yake kwenye msimamo wa Ligi

Pamba Jiji kumrejesha tena uwanjani Kelvin Yondani

Picha
Mara baada ya kumalizika kwa msimu 2023/24 akiwa na kikosi cha Geita Gold ambacho kwa bahati mbaya kilishuka daraja na sasa kinashiriki #championship, Mlinzi mkongwe Kelvin Yondani hakubahatika kuwa na timu ya kuitumikia kutokana na sababu mbalimbali. Miezi kadhaa imepita bila shoo za Yondani ndani ya #LigiKuu hatimaye wakazi wa Mwanza huenda wakashuhudia shoo za mtoto wao wa nyumbani kabisa tena katika timu ya barazani kwao yaani nyumbani kabisa. Klabu ya Pamba Jiji inatajwa kukamilisha usajili wa Mlinzi huyu wa maana kabisa kuwahi kuzitumikia klabu kongwe hapa nchini za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti, Kwa mujibu wa taarifa ni kuwa Yondani amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuipambania klabu ya Pamba Jiji.

Yacouba bado wa moto

Picha
Yacouba Sogne bado mpira upo sana mguuni, ana mabao manne (4) na assists tatu (3) jumla amehusika kwenye mabao saba (7) ya Tabora United. Namba 10 ya maana kabisa ya mpira wa miguu ana takwimu nzuri sana ndani ya NBC Premier League, hizi takwimu ni nzuri sana Mshambuliaji huyo leo amefunga bao moja licha kwamba timu yake imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC, goli lingine limefungwa na Offen Chikola

Ali Kamwe kuburuzwa mahakamani kisa kidomodomo chake

Picha
Kampuni ya Kisheria inayomsimamia Mfanyabiashara Sandaland the Only One ambaye ndie Mtengenezaji wa jezi za SIMBA imemtumia barua Meneja wa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ikidai fidia ya BILLION TATU kutokana na kauli za kumchafua Mteja wao na imepelekea kuathiri biashara zake. Wanadai Kamwe alitoa maneno kuwa Viongozi wa Simba wamemsema sana Sandaland kuwa wanatukanwa kisa yeye na wakamsusia uzinduzi wa jezi ndio maana akaenda kufanyia dukani kwake. Kwenye Demand Notice hiyo wanataka KAMWE afanye mambo yafuatayo: 1- Kulipa fidia ya 3,000,000,000 2- Kumwomba msamaha hadharani Sandaland kwa kumkashfu kuwa anazalisha jezi mbaya hazina ubora. 3- Anapaswa kuomba msamaha kwa Umma kupitia vyombo vya habari vile vile alivyotumia kuongea alichoongea. 4- Ana siku saba (7) za kufanya yote hayo nje na hapo hatua kali zaidi watazichukua.

Baka, Mzize na Aucho kuikosa Namungo kesho

Picha
Yanga itaendelea kuwakosa wachezaji wake Khalid Aucho, Clement Mzize ambao ni majeruhi na Ibrahim Bacca anaetumikia adhabu ya kadi nyekundu. Yanga SC tayari wapo Ruangwa, Lindi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Namungo FC utakao pigwa Novemba 30, jumamosi hii katika dimba la Majaliwa Stadium.

JKT Tanzania yaipapasa Fountain Gate

Picha
BAO la kiungo mkongwe wa umri wa miaka 31, Najim Magulu dakika ya 34 limeipa JKT Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.

Jahazi la Singida Black Stars lazidi kuzama

Picha
Jahazi la Singida Black Stars linazidi kuzama baada ya usiku huu kufungwa mabao 2-1 dhidi ya matajiri wa Chamazi, Azam FC mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam. Mabao mawili ya Feisal Salum au Feitoto dakika ya 38 na Jhonier Blanco dakika 57 yaliitanguliza timu hiyo uongozini ambayo sasa imefikisha pointi 27 ikiendelea kukaa nafasi ya pili, nyuma ya Simba SC wenye pointi 28. Bao la Singida Black Stars limefungwa na Elvis Rupia dakika 62, hali ya Singida Black Stars si nzuri kwani tayari imeshatimua makocha wake kutokana na matokeo mabaya inayopata.

Yanga mbioni kuukacha uwanja Mkapa

Picha
Baadhi ya wajumbe wa Klabu ya soka ya Young Africans, wanania ya kuwasilisha wazo kwenye kamati ya Klabu hiyo kuuacha uwanja wa taifa wa Benjamin Mkapa na kuelekea katika uwanja wa New Aman Complex Stadium. Visiwani Zanzibar. Sababu ambazo wanaona wao zina nguvu:- 1. Uchache wa mashabiki wa Klabu hiyo ambao wanajitokeza Benjamin Mkapa. 2. Wanaamini Uwanja mmoja unavyotumika na timu mbili kuna kuwa na hujuma tofauti tofauti. Bado kikao hakijafanyika, nitakujuza kadiri nitakavyo kuwa napenyezewa taarifa hiyo.

Bayo asaini miwili Yanga

Picha
Mshambuliaji ambaye ni raia wa Uganda, Fahad Bayo amesaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Yanga SC Kilichobaki anasubiri vibali kutoka TFF ambavyo Yanga SC wameambiwa vitatoka Jumatatu ijayo na ataanza kucheza mwezi ujao kuanzia tarehe 15.

Tanzania yapanda viwango FIFA

Picha
Tanzania imepanda nafasi sita (6) katika viwango vya ubora duniani [FIFA] kutoka nafasi ya 112 mpaka nafasi ya 106. Kenya wameporomoka kutoka nafasi ya 106 mpaka 108. Huku Uganda ndio wanaongoza kwa upande wa Afrika mashariki wakiwa nafasi ya 88.

Simba ikicheza vile, tano zitawahusu- Jemedari

Picha
Mchambuzi wa soka nchini Jemedari Said ameshangazwa na kiwango kibovu cha Simba SC dhidi ya Bravo's de Maquis ya Angola na amedai kwma wataendelea hivyo basi tutegemee kuona ikifungwa mabao matano matano. "Kama Simba Sc watacheza vile walivyocheza dhidi ya Bravos de Marquis dhidi ya timu nyingine katika kundi lao, naona kabisa wataturudisha kule katika kufungwa mabao matano matano, wanapaswa kubadilika kwa kiasi kikubwa“-Mchambuzi Jemedari Said

Gadiel Michael, Majogolo wang' ara Afrika Kusini

Picha
Nyota wa Tanzania Gadiel Michael na Baraka Majogoro wanaokipiga katika klabu ya Chippa United ya Afrika kusini jana walikuwa mzigoni katika mchezo wa Ligi Kuu ambao walipata alama moja dhidi ya SuperSport United

Siasa zimemuondoa Gamondi, Yanga

Picha
Na Prince Hoza MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga SC hivi karibuni walifanya maamuzi makubwa na ya kushitua nchi, baada ya kumfuta kazi kocha wake mkuu Miguel Angel Gamondi raia wa Argentina na msaidizi wake Moussa Ndaw raia wa Senegal. Yanga waliamua kumfuta kazi Gamondi na msaidizi wake baada ya mwenendo mbaya walioanza nao msimu huu, kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Azam FC na cha mabao 3-1 dhidi ya Tabora United kilitosha kabisa kuwafuta kazi wakuu hao wa benchi la ufundi. Kipigo hicho mfululizo ni cha kwanza kwao tangu walipoanza jukumu la kuiongoza timu hiyo iliyofanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Azam FC mabao 4-1 kwenye mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar. Tangu kuanza kwa msimu huu, Yanga imewachukua mechi ya tisa na ya kumi kupoteza, timu hiyo ilicheza mechi nane mfululizo ikipata ushindi na iliweka rekodi ya kipekee ya kutoruhusu bao hata moja kupenya kwenye nyavu zake. Lakini mwenendo wa kikosi hicho msimu huu haukuvuti...

Kipresha atetea kiti chake Mdaula

Picha
Mwenyekiti wa kijiji cha Mdaula, Chalinze mkoani Pwani kupitia CCM, Shabani Hussein "Kipresha" ametetea kiti chake baada ya kumshinda vibaya mgombea wa CHADEMA Kassim Ramadhan Kondo. Kipresha ambaye pia ni kocha wa soka daraja C, ameshinda kwa kura 1866 wakati mpinzani wake amepata kura 23 tu. Akipokea ushindi huo, Kipresha amesema Wanamdaula wameridhishwa na uongozi wake kutokana na kutimiza dhamila aliyokuwa nayo ikiwemo kutekeleza miradi ya kimaendeleo Shabani Hussein Kipresha ametetea kiti chake Mdaula

Pambano la Tyson na Jake lavunja rekodi

Picha
Pambano la ndondi la Jake Paul na Mike Tyson kwenye Uwanja wa AT&T limevunja rekodi baada ya kuhudhuriwa na watu 72,300, na hivyo kuzalisha mauzo ya tiketi ya Dola Milioni 18. [Tsh Bilioni 47.6] mauzo ambayo ni ya juu zaidi kwa michezo ya mapigano yote yaliyowahi kufanyika nje ya mji wa Las Vegas. Mapato makubwa ya kifedha kwa pambano hilo ni historia kubwa kwa Jake Paul na Mike Tyson mbali na hayo, pambano hilo limeingia kwenye historia ya pambano la ndondi la dau kubwa zaidi katika vitabu vingi vya michezo.

Percy Tau akataa mamilioni ya kuvunja mkataba Al Ahly

Picha
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Afrika Kusini na Klabu ya Al Ahly ya Misri Percy Tau (30) ameikataa ofa ya USD 300,000 (Tsh milioni 797) ya Al Ahly ili akubali kuvunjiwa Mkataba wake mwezi January na kuondoka kama mchezaji huru. Tau hana tatizo na kuvunjiwa mkataba wake ila anataka alipwe USD 600,000 (Tsh Bilioni 1.5), Tau aliyejiunga na Al Ahly 2021 akitokea Brighton ya England Mkataba wake na Al Ahly unaisha mwisho wa msimu 2024/2025. Inaelezwa kuwa Tau anataka Al Ahly kuvunja Mkataba kwa kufuata taratibu ya kumlipa mshahara wake wote wa miezi sita (ambao ni USD 100,000 kwa mwezna) na sio kulipwa mshahara wa miezi mitatu.

Simba hawataki utani, yailaza Bravo's 1-0

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC hawatanii kwenye michuano ya kimataifa baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravo's de Maquis mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili, kipa Mguinea wa Simba, Moussa Camara aliokoa mkwaju wa penalti wa mshambuliaji Mnigeria wa Bravos do Maquis, Emmanuel Edmond na kuwanusuru wenyeji kuruhusu bao. Bao pekee limefungwa na Jean Charles Ahoua dakika ya 26, kwa matokeo hayo Simba sasa imefikisha pointi 3 na kuanza vema michuano hiyo ya pili kwa ukubwa. Jana watani zao Yanga SC walikubali kichapo cha mabao 2-0 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na kuwaudhi mashabiki wake.

Kocha Yanga awachoma wachezaji wake

Picha
Wakati maandalizi kuelekea mchezo wa Jumanne dhidi ya Al Hilal (CAFCL) ukiendelea AVIC TOWN, Kocha wa Yanga SC, Saed Ramovic ameweka wazi kuwa mchezo anaoutaka ni wa kasi, na kuwasumbua wapinzani wasipate muda wa kupumua. Akiongea na Mwanaspoti, Ramovic ameeleza, "kwa sasa tunachotaka ni kucheza kwa kasi, kuwasumbua wapinzani wasiwe na muda wa kupumua kujiuliza wamekosea wapi?." Falsafa yenyewe ikiwa ni kushambulia mwanzo mwisho. Ramovic amewasihi Mashabiki wawe wavumilivu kwani ni zoezi la muda ambalo haliwezi kukamilika kwa muda mfupi kama matarajio ya watu yalivyo

Shabiki aliyekodi ndege binafsi kuiona Yanga azua balaa

Picha
Shabiki wa Yanga Said Mohamed Hassan Hapo Jana Alikodi Ndege Binafsi kutoka mkoani Arusha Hadi Dar es salaam na baadae kumrudisha Tena Arusha kwaajili ya Kwenda kuangalia Timu yake ya Yanga ikicheza dhidi ya Alhilal "Mimi naitwa Mr Said mohamed hassan ni Shabiki wa Yanga, kipindi kile yanga omba omba tulijitahidi sana kuishika mkono timu yetu tunakamata madaftari tunachangisha michango kwaajili ya furaha ya yanga tulitegemea kipindi hichi wamekuja wakina Hersi watupe furaha" "kipindi kile tunatoa michango yetu yanga itupe furaha sasa hivi yanga haina shida Yeyote lakini inatupa maumivu makubwa hivi Leo nimetoka Arusha hadi hapa nimekodi Ndege Private dollar 3000 mpaka hapa kwenda na Kurudi piga hesabu ni shingapi hizo" "Unatoa pesa hiyo unakuja kuangalia mechi halafu timu inapoteza inaumiza sana, inachotakiwa viongozi wakae chini waijue yanga ina nini wachezaji wananini na wana shida gani mbona ile yanga ombaomba haikuwahi kufungwa mechi tatu mfululizo" ...

Gamondi aishukuru Yanga

Picha
Aliyekuwa Kocha wa Klabu ya Yanga Miguel Gamondi Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameishukuru Klabu ya Yanga kwa Mara ya Kwanza baada ya Kumalizana na Vigogo ha wa Jangwani. Gamondi amechapisha ujumbe unaosema; “Thank you very Much Asante sana Wananchi , To My Players , and Everybody , .. I am Very Gratefull and Proud to be Part of Yanga in My Time You will always be in my heart, Much Love”

Rasmi, Gamondi amalizana na Singida

Picha
Klabu ya Singida Black Stars imefikia makubaliano na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga SC, Miguel Gamondi kuwa kocha wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili. Gamondi- alitimuliwa na Yanga SC aliyosaini nayo mkataba wa mwaka mmoja ambao unamalizika mwishoni mwa msimu. Mambo Uwanjani Blog mapema Leo iliandika tetesi za ujio wa Gamondi na hatimaye dili limetiki. Karibu tena Gamondi Tanzania

Ramovic aomba apewe wiki 4 kuirudisha Yanga kiubora

Picha
Kocha mkuu wa Yanga SC, Sead Ramovic ameikatia tamaa timu yake ya Yanga SC huku akiomba apewe wiki 3 au 4 ili ahakikishe fitness level ya wachezaji ikae sawa kwani amegundua fitiness level haipo. "Niliyoiona timu yangu uwanjani katika fitness level ipo chini yani na sikubwa, tunahitaji wiki 3 au 4 ili kuipata fitness level ambayo naiitaji, kwa hizi mechi za katikati tutajua cha kufanya lakini ni ngumu sana kufikia malengo yetu". Alisema Sead Ramovic, Kocha Mkuu wa Yanga SC via Azam TV. Sead Ramovic

Al Hilal yatonesha kidonda Yanga

Picha
Hali si shwari kwa Wananchi, jioni ya leo imekubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya mashabiki wake katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam dhidi ya Al Hilal Omduman ya Sudan mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika. Hicho ni kipigo cha tatu mfululizo, baada ya vipigo viwili vya kwenye Ligi Kuu bara 1-0 dhidi ya Azam FC na 3-1 dhidi ya Tabora United na kumtimua kocha wake Miguel Gamondi-. Leo ilikuwa mechi ya kwanza ya kocha mpya wa mabingwa hao wa bara, Sead Ramovic raia wa Ujerumani na imekuwa ngumu kwa kukubali kichapo. Mabao ya Al Hilal ambao sasa watakuwa kileleni kwenye kundi lao lenye timu za TP Mazembe na MC Alger, yalifungwa na Adama Coulibaly dakika ya 63 na Yassir Mozamil dakika ya 90

Poul Pogba na ndugu zake hawapikiki chungu kimoja

Picha
Mchezaji maarufu duniani Paul Pogba,ana kaka zake wawili Mathias na Florentin Pogba,wote ni wachezaji Ila ndugu zake hawafanikiwa kucheza ligi kubwa na timu kubwa Kama Paul Pogba. Paul Pogba na ndugu yake Mathias Pogba hawapikiki chungu kimoja kutokana na masuala ya kifedha, Mwaka 2022 Mathias Pogba alimtuhumu Paul Pogba kutumia pesa vibaya na kumnyima haki Kama ndugu na alikwenda mbali akimtuhumu kutumia ushirikina kupata mafanikio ya kisoka. Paul Pogba,alijibu Kwa kusema Kuna muda anatamani asingekuwa na fedha,kwani zimemtenganisha na ndugu na jamaa,kwani wengi wanaamini anapesa nyingi na anachotoa ni kichache Kama msaada,Kuna nyakati ndugu yake Mathias alikodi wahuni wakamteka na kudai awape Euro milioni kumi na tatu.

Gamondi kumrithi Aussems, Singida Black Stars

Picha
Baada ya klabu ya Singida Black Stars kumfungashia virago kocha wake mkuu Patrick Aussems pamoja na msaidizi wake Denis Kitambi, tayari klabu hiyo imeanza mazungumzo na makocha kadhaa ili kurithi nafasi hiyo. Kocha aliyefurushwa na Yanga SC hivi karibuni, Miguel Gamondi raia wa Argentina anatajwa kuwa kwenye rada za klabu hiyo na ikiwezekana atarejea tena kwenye ligi hiyo kuendelea na majukumu yake. Yanga ilimfuta kazi Gamondi baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya Azam FC na Tabora United, Wanangwani hao waliamua kumtimua kazi Gamondi na msaidizi wake Moussa Ndaw raia wa Senegal, Yanga ikifungwa 1-0 na Azam FC na 3-1 na Tabora United. Miguel Gamondi

TP Mazembe ya wanawake yatwaa ubingwa wa Ligi ya mabingwa

Picha
Klabu ya TP Mazembe ya wanawake ndio mabingwa wapya wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake baada ya kuwapiga AS FAR kichapo cha bao 1-0. Mazembe wanafikia rekodi ya Mamelodi kwa kutwaa Kombe hilo mara mbili.

Simba yaifanyia umafia Yanga

Picha
Kuna uwezekano mkubwa msimu ujao kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua wa Yanga SC akatimkia kwa watani wao Simba SC baada ya kuwagomea kuongeza mkataba mpya. Pacome amekataa kuongeza mkataba mwingine akidai kwamba tayari kuna timu ameshafanya nayo mazungumzo na ofa yao ni nzuri hivyo anataka kuondoka ukimalizika mkataba wake. Ingawa hakuwa tayari kuitaja klabu hiyo aliyofanya nayo mazungumzo, chanzo chetu kimebaini kuwa ni Simba, kwani ndio timu iliyokuwa ikimuhitaji.

Aussems, Kitambi wafungashiwa virago Singida Black Stars

Picha
Uongozi wa klabu ya Singida Black Stars umemfuta kazi kocha wake mkuu Patrick Aussems pamoja na msaidizi wake Denis Kitambi kutokana na matokeo yasioridhisha katika michezo yao ya ligi kuu ya NBC. Gamondi alifungashiwa virago katika klabu ya Yanga huku mchezo wake wa mwisho ulikuwa ni dhidi ya Tabora UTD ambapo alipata matokeo mabovu, na vile vile hii leo kocha Patrick Aussems amefutwa kazi baada ya kucheza na Tabora UTD na kuambulia sare ya mabao 2-2.

MO Salah kutimka mwishoni mwa msimu

Picha
Nyota wa Liverpool raia wa Misri Mo Salah amesema anakaribia kuondoka klabuni hapo kutokana na mkataba wake kufikia ukingoni “Tayari tunaikaribia Disemba lakini sijapokea ofa yeyote mpaka sasa ya kuongeza mkataba na kuendelea kusalia hapa , naipenda sana Liverpool nawapenda mashabiki wake na kwangu mimi haijawahi kutokea klabu bora kama Liverpool lakini mwisho wasiku hili lipo nje ya uwezo wangu’’ Mo Salah Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 mkataba wake utafika tamati Juni 2025 alijiunga na Liverpool 2017 akitokea AS Roma mpaka sasa ameisaidia klabu yake kubeba EPL 2020, UCL 2019 na msimu huu amecheza mechi zote 12 ndani ya EPL huku akifunga magoli 10 na assist 6 na kuiweka klabu yake kileleni mwa msimamo wa ligi.

CAF yaidhibu Tanzania

Picha
CAF imethibitisha kuwa Tanzania itashiriki michuano ijayo ya AFCON 2025 lakini Tanzania imepigwa faini ya USD 50000 (Tshs 132m) kwa kosa la Mchezaji wao kutumia namba mbili tofauti Pia CAF imetupilia mbali malalamiko ya Shirikisho la Soka la Guinea kuhusu ombi lao la kuhitaji Tanzania iondolewe katika michuano ya AFCON 2025 kutokana na Mchezaji wao kutumia namba mbili tofauti.

Tabora United yaishika shati Singida BS

Picha
Timu ya Tabora United ya mkoani Tabora imepambana vya kutosha na kufanikiwa kusawazisha mabao yote mawili na kuwa sare ya mabao 2-2 dhidj ya Singida Black Stars mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Singida Black Stars itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kulinda mabao yake mawili iliyoyapa kupitia Elvis Rulla dakika ya 16 na Antonu Trabi Tra dakika ya 32. Heritier Makambo alikuwa mwiba kwa Singida na kuisawazishia bao Tabora United.

Ibenge aingia mchecheto kwa Yanga

Picha
Kocha mkuu wa Al Hilal Omduman ya Sudan, Frolient Ibenge raia wa DR Congo ameonesha hofu na kikosi cha sasa cha Yanga SC ambao watakutana nao kesho. "Yanga inawachezaji wazuri sana ambao wanaweza kucheza timu yoyote hapa Africa, unapoenda kukutana na timu kama hiyo lazima ujipange kukukabiliana naamini kesho tutakuwa na mechi ngumu," . "Hatujui Yanga wanacheza huo ndio ugumu wa mchezo huu unapokuja,hatujui mbinu za kocha wao mpya anachezaje,tunaenda na tahadhari kubwa sana juu yao," Frolient Ibenge kocha Mkuu wa Klabu ya Al Hilal.

Mastaa wa Tanzania wazibeba timu zao Ulaya

Picha
Nyota wa Tanzania Kelvin John anayecheza katika klabu ya Aalborg ya Denmark ameisaidia timu yake kupata alama moja kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika kwa sare 0:0 dhidi ya Viborg FC. Nyota wa Tanzania Novatus Dismas Miroshi ameisaidia timu ya Gotzepe ya Uturuki kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Besiktas katika mchezo wa Ligi Kuu

Fadlu humwambii kitu kwa Chasambi

Picha
Kocha wa Simba SC Fadlu Davids kwasasa humwambii kitu kwa kiungo mshambuliaji wa kioosi hicho Ladack Chasambi na amedai anampenda sana kutokana na kiwango chake. Awali Fadlu raia wa Afrika Kusini alikuwa hamwelewi Chasambi na alikuwa anamweka benchi, kocha huyo alipendelea kumpanga Edwin Balua upande wa kulia na Kibu Denis au Mutale. Lakini sasa kocha huyo humwambii kitu kwa Chasambi na anaamini kwamba kiungo mshambuliaji huyo ana kitu kikubwa mguuni mwake

Al Hilal yamuhofia Maxi Nzengeli

Picha
Mchezaji hatari ndani ya Yanga SC ni Maxi Mpia Nzengeli,Ndiyo mchezaji mgumu pekee atakayetupa wakati mgumu ndani ya uwanja na mtaona haya pale akipata nafasi ya kucheza. Jean Claude Girumgisha winga wa Al Hilal leo ameweka wazi mchezaji ambaye atawasumbua zaidi jumanne katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Niko tofauti na Gamondi- Ramovic

Picha
Kocha wa Yanga SC Sead Ramovic ameweka wazi kwamba yeye staili yake ya uchezaji upo tofauti kidogo na mtangulizi wake Miguel Gamondi. "Mtindo wangu wa uchezaji upo tofauti kidogo, napenda sana kujilinda vizuri na kushambulia sana, kumfinya Mpinzani kiasi ambacho simpi nafasi ya kupumua, aina hii ya mchezo huchukua muda na jitihada ila nawaahidi kwa Wachezaji hawa na kikosi hiki tukishafikia hapo basi kuitazama Yanga Afrika itakuwa ni starehe, hilo nawaahidi” - Saed Ramovic, Kocha Mkuu wa Yanga

Simba yakubali yaishe kwa Lakred

Picha
Uongozi wa klabu ya Simba upo tayari kumwachia Mlinda lango wao Ayoub Lakred kwenye dirisha dogo la usajili, Ayoub ambaye alikuwa nje ya Uwanja kutokana na kuwa majeruhi tangu msimu huu uanze na sasa ameshapona na amekwisha anza mazoezi na wenzake, Kabla ya kupata Majeraha Mlinda lango Ayoub aliwahi kuhitajika na vilabu vya JS Kabylie ya Algeria na Raja Casablanca ya Morocco, Kwasasa Simba Sc ina walinda lango 6 Moussa Pinpin Camara Aishi Manula Ally Salim Hussein Abel Ayoub Lakread Ahmad Feruz.

Mtanzania ang' ara Morocco

Picha
Nyota wa Tanzania Jaruph Juma ameisaidia timu yake ya Ain Diab kupata ushindi wa magoli 5-0 kwenye mchezo wa Ligi kuu ya Soka la Ufukweni ya Morocco (Beach Soccer) dhidi ya timu ya Hercules. Jaruph amefunga magoli 3 katika mchezo huo. hii inadhihirisha kwamba wachezaji wa Tanzania wanafanya vizuri nje.

Azam FC yailaza Kagera Sugar 1-0

Picha
Timu ya Azam FC usiku huu imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Azam Complex mchezo wa Ligi Kuu bara. Bao pekee la Azam limefungwa na kinara wake wa mabao msimu uliopita Feisal Salum "Feitoto", kwa ushindi huo Azam imefikisha pointi 24 ikiwa sawa na Yanga SC.