Ramovic aomba apewe wiki 4 kuirudisha Yanga kiubora
Kocha mkuu wa Yanga SC, Sead Ramovic ameikatia tamaa timu yake ya Yanga SC huku akiomba apewe wiki 3 au 4 ili ahakikishe fitness level ya wachezaji ikae sawa kwani amegundua fitiness level haipo.
"Niliyoiona timu yangu uwanjani katika fitness level ipo chini yani na sikubwa, tunahitaji wiki 3 au 4 ili kuipata fitness level ambayo naiitaji, kwa hizi mechi za katikati tutajua cha kufanya lakini ni ngumu sana kufikia malengo yetu".
Alisema Sead Ramovic, Kocha Mkuu wa Yanga SC via Azam TV.