Simba hawataki utani, yailaza Bravo's 1-0

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC hawatanii kwenye michuano ya kimataifa baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravo's de Maquis mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili, kipa Mguinea wa Simba, Moussa Camara aliokoa mkwaju wa penalti wa mshambuliaji Mnigeria wa Bravos do Maquis, Emmanuel Edmond na kuwanusuru wenyeji kuruhusu bao.

Bao pekee limefungwa na Jean Charles Ahoua dakika ya 26, kwa matokeo hayo Simba sasa imefikisha pointi 3 na kuanza vema michuano hiyo ya pili kwa ukubwa.

Jana watani zao Yanga SC walikubali kichapo cha mabao 2-0 katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na kuwaudhi mashabiki wake.




Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA