Percy Tau akataa mamilioni ya kuvunja mkataba Al Ahly

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Afrika Kusini na Klabu ya Al Ahly ya Misri Percy Tau (30) ameikataa ofa ya USD 300,000 (Tsh milioni 797) ya Al Ahly ili akubali kuvunjiwa Mkataba wake mwezi January na kuondoka kama mchezaji huru.

Tau hana tatizo na kuvunjiwa mkataba wake ila anataka alipwe USD 600,000 (Tsh Bilioni 1.5), Tau aliyejiunga na Al Ahly 2021 akitokea Brighton ya England Mkataba wake na Al Ahly unaisha mwisho wa msimu 2024/2025.

Inaelezwa kuwa Tau anataka Al Ahly kuvunja Mkataba kwa kufuata taratibu ya kumlipa mshahara wake wote wa miezi sita (ambao ni USD 100,000 kwa mwezna) na sio kulipwa mshahara wa miezi mitatu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA