Shabiki aliyekodi ndege binafsi kuiona Yanga azua balaa
Shabiki wa Yanga Said Mohamed Hassan Hapo Jana Alikodi Ndege Binafsi kutoka mkoani Arusha Hadi Dar es salaam na baadae kumrudisha Tena Arusha kwaajili ya Kwenda kuangalia Timu yake ya Yanga ikicheza dhidi ya Alhilal
"Mimi naitwa Mr Said mohamed hassan ni Shabiki wa Yanga, kipindi kile yanga omba omba tulijitahidi sana kuishika mkono timu yetu tunakamata madaftari tunachangisha michango kwaajili ya furaha ya yanga tulitegemea kipindi hichi wamekuja wakina Hersi watupe furaha"
"kipindi kile tunatoa michango yetu yanga itupe furaha sasa hivi yanga haina shida Yeyote lakini inatupa maumivu makubwa hivi Leo nimetoka Arusha hadi hapa nimekodi Ndege Private dollar 3000 mpaka hapa kwenda na Kurudi piga hesabu ni shingapi hizo"
"Unatoa pesa hiyo unakuja kuangalia mechi halafu timu inapoteza inaumiza sana, inachotakiwa viongozi wakae chini waijue yanga ina nini wachezaji wananini na wana shida gani mbona ile yanga ombaomba haikuwahi kufungwa mechi tatu mfululizo"
"Nimekuwa nikiisapoti Yanga sana popote inapokwenda, kwenye Mchezo na Belouzdad nilifunga Safari Kwa Gharama zangu na pia kwenye fainali ya kombe la Shirikisho nililipia ndege Kila kitu malazi kwenda kuiona Yanga lakini tulitoka tumeridhika Yanga haikufungwa Michezo mfululizo kama msimu huu"