Azam FC yailaza Kagera Sugar 1-0
Timu ya Azam FC usiku huu imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Azam Complex mchezo wa Ligi Kuu bara.
Bao pekee la Azam limefungwa na kinara wake wa mabao msimu uliopita Feisal Salum "Feitoto", kwa ushindi huo Azam imefikisha pointi 24 ikiwa sawa na Yanga SC.