Jahazi la Singida Black Stars lazidi kuzama
Jahazi la Singida Black Stars linazidi kuzama baada ya usiku huu kufungwa mabao 2-1 dhidi ya matajiri wa Chamazi, Azam FC mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mabao mawili ya Feisal Salum au Feitoto dakika ya 38 na Jhonier Blanco dakika 57 yaliitanguliza timu hiyo uongozini ambayo sasa imefikisha pointi 27 ikiendelea kukaa nafasi ya pili, nyuma ya Simba SC wenye pointi 28.
Bao la Singida Black Stars limefungwa na Elvis Rupia dakika 62, hali ya Singida Black Stars si nzuri kwani tayari imeshatimua makocha wake kutokana na matokeo mabaya inayopata.