MO Salah kutimka mwishoni mwa msimu
Nyota wa Liverpool raia wa Misri Mo Salah amesema anakaribia kuondoka klabuni hapo kutokana na mkataba wake kufikia ukingoni
“Tayari tunaikaribia Disemba lakini sijapokea ofa yeyote mpaka sasa ya kuongeza mkataba na kuendelea kusalia hapa , naipenda sana Liverpool nawapenda mashabiki wake na kwangu mimi haijawahi kutokea klabu bora kama Liverpool lakini mwisho wasiku hili lipo nje ya uwezo wangu’’ Mo Salah
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 mkataba wake utafika tamati Juni 2025 alijiunga na Liverpool 2017 akitokea AS Roma mpaka sasa ameisaidia klabu yake kubeba EPL 2020, UCL 2019 na msimu huu amecheza mechi zote 12 ndani ya EPL huku akifunga magoli 10 na assist 6 na kuiweka klabu yake kileleni mwa msimamo wa ligi.