Al Hilal yatonesha kidonda Yanga
Hali si shwari kwa Wananchi, jioni ya leo imekubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya mashabiki wake katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam dhidi ya Al Hilal Omduman ya Sudan mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika.
Hicho ni kipigo cha tatu mfululizo, baada ya vipigo viwili vya kwenye Ligi Kuu bara 1-0 dhidi ya Azam FC na 3-1 dhidi ya Tabora United na kumtimua kocha wake Miguel Gamondi-.
Leo ilikuwa mechi ya kwanza ya kocha mpya wa mabingwa hao wa bara, Sead Ramovic raia wa Ujerumani na imekuwa ngumu kwa kukubali kichapo.
Mabao ya Al Hilal ambao sasa watakuwa kileleni kwenye kundi lao lenye timu za TP Mazembe na MC Alger, yalifungwa na Adama Coulibaly dakika ya 63 na Yassir Mozamil dakika ya 90