Fadlu humwambii kitu kwa Chasambi
Kocha wa Simba SC Fadlu Davids kwasasa humwambii kitu kwa kiungo mshambuliaji wa kioosi hicho Ladack Chasambi na amedai anampenda sana kutokana na kiwango chake.
Awali Fadlu raia wa Afrika Kusini alikuwa hamwelewi Chasambi na alikuwa anamweka benchi, kocha huyo alipendelea kumpanga Edwin Balua upande wa kulia na Kibu Denis au Mutale.
Lakini sasa kocha huyo humwambii kitu kwa Chasambi na anaamini kwamba kiungo mshambuliaji huyo ana kitu kikubwa mguuni mwake