Mtibwa Sugar kurejea Ligi Kuu
Timu ya Mtibwa Sugar wanaendelea kufanya vizuri kwenye ligi ya Championship baada ya kuilaza Mbuni mwbwo 2-0 huku ikiwa imeshinda mchezo wa nane kati ya 11 iliyocheza.
Juma Luizio dakika ya 31 alitangulia kuifungia bao la kwanza kabla ya Anuary Jabir dakika ya 69 kufunga bao la pili.
TAKWIMU ZA MTIBWA KAMA ZILIVYO
11 Mechi
08 Ushindi
02 Sare
01 Vipigo
19 Magoli ya kufunga
05 Magoli ya kufungwa
07 Clean Sheet
Kwasasa iko kileleni
.