Simba yaifanyia umafia Yanga
Kuna uwezekano mkubwa msimu ujao kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua wa Yanga SC akatimkia kwa watani wao Simba SC baada ya kuwagomea kuongeza mkataba mpya.
Pacome amekataa kuongeza mkataba mwingine akidai kwamba tayari kuna timu ameshafanya nayo mazungumzo na ofa yao ni nzuri hivyo anataka kuondoka ukimalizika mkataba wake.
Ingawa hakuwa tayari kuitaja klabu hiyo aliyofanya nayo mazungumzo, chanzo chetu kimebaini kuwa ni Simba, kwani ndio timu iliyokuwa ikimuhitaji.