Gamondi kumrithi Aussems, Singida Black Stars
Baada ya klabu ya Singida Black Stars kumfungashia virago kocha wake mkuu Patrick Aussems pamoja na msaidizi wake Denis Kitambi, tayari klabu hiyo imeanza mazungumzo na makocha kadhaa ili kurithi nafasi hiyo.
Kocha aliyefurushwa na Yanga SC hivi karibuni, Miguel Gamondi raia wa Argentina anatajwa kuwa kwenye rada za klabu hiyo na ikiwezekana atarejea tena kwenye ligi hiyo kuendelea na majukumu yake.
Yanga ilimfuta kazi Gamondi baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya Azam FC na Tabora United, Wanangwani hao waliamua kumtimua kazi Gamondi na msaidizi wake Moussa Ndaw raia wa Senegal, Yanga ikifungwa 1-0 na Azam FC na 3-1 na Tabora United.