Pamba Jiji kumrejesha tena uwanjani Kelvin Yondani

Mara baada ya kumalizika kwa msimu 2023/24 akiwa na kikosi cha Geita Gold ambacho kwa bahati mbaya kilishuka daraja na sasa kinashiriki #championship, Mlinzi mkongwe Kelvin Yondani hakubahatika kuwa na timu ya kuitumikia kutokana na sababu mbalimbali.

Miezi kadhaa imepita bila shoo za Yondani ndani ya #LigiKuu hatimaye wakazi wa Mwanza huenda wakashuhudia shoo za mtoto wao wa nyumbani kabisa tena katika timu ya barazani kwao yaani nyumbani kabisa.

Klabu ya Pamba Jiji inatajwa kukamilisha usajili wa Mlinzi huyu wa maana kabisa kuwahi kuzitumikia klabu kongwe hapa nchini za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti,

Kwa mujibu wa taarifa ni kuwa Yondani amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuipambania klabu ya Pamba Jiji.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA