Niko tofauti na Gamondi- Ramovic
Kocha wa Yanga SC Sead Ramovic ameweka wazi kwamba yeye staili yake ya uchezaji upo tofauti kidogo na mtangulizi wake Miguel Gamondi.
"Mtindo wangu wa uchezaji upo tofauti kidogo, napenda sana kujilinda vizuri na kushambulia sana, kumfinya Mpinzani kiasi ambacho simpi nafasi ya kupumua, aina hii ya mchezo huchukua muda na jitihada ila nawaahidi kwa Wachezaji hawa na kikosi hiki tukishafikia hapo basi kuitazama Yanga Afrika itakuwa ni starehe, hilo nawaahidi”
- Saed Ramovic, Kocha Mkuu wa Yanga