Chama, Aziz Ki wanahitaji kuongezewa ubora
Kocha mkuu wa Yanga SC Sead Ramovic raia wa Ujerumani amesema wachezaji wake wawili Clatous Chama na Stephanie Aziz Ki ni wazuri ila wanahitaji kuongezewa ubora ama sivyo watapotea.
'Wapinzani wetu walikuwa wagumu nawapongeza,tumepata alama tatu ila bado napaswa kuongeza baadhi ya vitu kama vile fitness na vitu vingine taratibu taratibu.
Chama na Aziz wote ni wachezaji wazuri japo napaswa kuwaongezea ubora wao hasa fitness", amesema Ramovic
.