Kocha Yanga awachoma wachezaji wake
Wakati maandalizi kuelekea mchezo wa Jumanne dhidi ya Al Hilal (CAFCL) ukiendelea AVIC TOWN, Kocha wa Yanga SC, Saed Ramovic ameweka wazi kuwa mchezo anaoutaka ni wa kasi, na kuwasumbua wapinzani wasipate muda wa kupumua.
Akiongea na Mwanaspoti, Ramovic ameeleza, "kwa sasa tunachotaka ni kucheza kwa kasi, kuwasumbua wapinzani wasiwe na muda wa kupumua kujiuliza wamekosea wapi?." Falsafa yenyewe ikiwa ni kushambulia mwanzo mwisho.
Ramovic amewasihi Mashabiki wawe wavumilivu kwani ni zoezi la muda ambalo haliwezi kukamilika kwa muda mfupi kama matarajio ya watu yalivyo