Tabora United yaishika shati Singida BS
Timu ya Tabora United ya mkoani Tabora imepambana vya kutosha na kufanikiwa kusawazisha mabao yote mawili na kuwa sare ya mabao 2-2 dhidj ya Singida Black Stars mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Singida Black Stars itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kulinda mabao yake mawili iliyoyapa kupitia Elvis Rulla dakika ya 16 na Antonu Trabi Tra dakika ya 32.
Heritier Makambo alikuwa mwiba kwa Singida na kuisawazishia bao Tabora United.