Pambano la Tyson na Jake lavunja rekodi
Pambano la ndondi la Jake Paul na Mike Tyson kwenye Uwanja wa AT&T limevunja rekodi baada ya kuhudhuriwa na watu 72,300, na hivyo kuzalisha mauzo ya tiketi ya Dola Milioni 18. [Tsh Bilioni 47.6] mauzo ambayo ni ya juu zaidi kwa michezo ya mapigano yote yaliyowahi kufanyika nje ya mji wa Las Vegas.
Mapato makubwa ya kifedha kwa pambano hilo ni historia kubwa kwa Jake Paul na Mike Tyson mbali na hayo, pambano hilo limeingia kwenye historia ya pambano la ndondi la dau kubwa zaidi katika vitabu vingi vya michezo.