Yanga mbioni kuukacha uwanja Mkapa
Baadhi ya wajumbe wa Klabu ya soka ya Young Africans, wanania ya kuwasilisha wazo kwenye kamati ya Klabu hiyo kuuacha uwanja wa taifa wa Benjamin Mkapa na kuelekea katika uwanja wa New Aman Complex Stadium. Visiwani Zanzibar.
Sababu ambazo wanaona wao zina nguvu:-
1. Uchache wa mashabiki wa Klabu hiyo ambao wanajitokeza Benjamin Mkapa.
2. Wanaamini Uwanja mmoja unavyotumika na timu mbili kuna kuwa na hujuma tofauti tofauti.
Bado kikao hakijafanyika, nitakujuza kadiri nitakavyo kuwa napenyezewa taarifa hiyo.