Yanga yaamkia Ruangwa
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC usiku huu imeamka usingizini mikononi mwa Namungo FC baada ya kuilaza mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa mkoani Lindi.
Kwa ushindi huo sasa Yanga imrfikisha pointi 27 ikiendelea kuifukuza Simba iliyo kileleni kwa tofauti ya alama moja.
Kennedy Musonda dakika ya 49 aliwaamsha mashabiki wa Yanga kabla ya Pacome Zouzoua dakika ya 68 kuongeza bao la pili, Namungo FC inayonolewa na Juma Mgunda imeendelea kufanya vibaya na kuhatarisha nafasi yake kwenye msimamo wa Ligi