Poul Pogba na ndugu zake hawapikiki chungu kimoja
Mchezaji maarufu duniani Paul Pogba,ana kaka zake wawili Mathias na Florentin Pogba,wote ni wachezaji Ila ndugu zake hawafanikiwa kucheza ligi kubwa na timu kubwa Kama Paul Pogba.
Paul Pogba na ndugu yake Mathias Pogba hawapikiki chungu kimoja kutokana na masuala ya kifedha, Mwaka 2022 Mathias Pogba alimtuhumu Paul Pogba kutumia pesa vibaya na kumnyima haki Kama ndugu na alikwenda mbali akimtuhumu kutumia ushirikina kupata mafanikio ya kisoka.
Paul Pogba,alijibu Kwa kusema Kuna muda anatamani asingekuwa na fedha,kwani zimemtenganisha na ndugu na jamaa,kwani wengi wanaamini anapesa nyingi na anachotoa ni kichache Kama msaada,Kuna nyakati ndugu yake Mathias alikodi wahuni wakamteka na kudai awape Euro milioni kumi na tatu.