Aussems, Kitambi wafungashiwa virago Singida Black Stars
Uongozi wa klabu ya Singida Black Stars umemfuta kazi kocha wake mkuu Patrick Aussems pamoja na msaidizi wake Denis Kitambi kutokana na matokeo yasioridhisha katika michezo yao ya ligi kuu ya NBC.
Gamondi alifungashiwa virago katika klabu ya Yanga huku mchezo wake wa mwisho ulikuwa ni dhidi ya Tabora UTD ambapo alipata matokeo mabovu, na vile vile hii leo kocha Patrick Aussems amefutwa kazi baada ya kucheza na Tabora UTD na kuambulia sare ya mabao 2-2.