Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2024

Kelvin John ajiunga timu ya Ligi Kuu Denmark

Picha
Mshambuliajia wa Taifa Stars anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji Kelvin John (20) amesaini Mkataba wa miaka minne kuichezea Klabu ya Aalborg FC iliyopanda daraja na sasa itacheza Ligi Kuu ya Denmark msimu wa 2024/2025. Kelvin alijiunga na KRC Genk 2021 na baadae kupandishwa timu ya wakubwa 2022 ila hakupata nafasi sana ya kucheza.

Mwijaku naye atambulishwa Crown FM

Picha
Kituo kipya cha redio kinahomilikiwa staa wa bongofleva Alikiba, Crown FM 92.1, kimeendelea kujimarisha baada ya kumjumuhisha Mwijaku. Tayari kituo hicho kinachosubiriwa kushusha burudani na ushindani kwa vituo vingine kimeorodhesha mastaa wengine kwenye utangazaji waliojiunga nacho. Mastaa ni pamoja na: ◉ Salim Kikeke (Huru) ◉ George Job from Wasafi fm. ◉ Hans Raphael from Wasafi fm. ◉ Nassib Mkomwa from Clouds fm ◉ DC Mwijaku from Clouds fm. ◉ Juma Ayo from Kishamba media

Bwalya na Wydad kimeeleweka

Picha
Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Nkana Rangers ya Zambia, Al Ahly ya Misri na Wydad Casablanca ya Morocco, Walter Bwalya ameamua kuondoa kesi yake FIFA na kukubaliana kuvunja mkataba. Bwalya aliishitaki Wydad Casablanca, FIFA, lakini amekaa chini na kuongea na viongozi wa klabu hiyo hatimaye wamekubaliana kumalizana hivyo akaamua kuondoa kesi hiyo na klabu ikaamua kuvunja mkataba wake Kwasasa Bwalya Ni mchezaji huru na anaweza kujiunga na klabu yoyote anayoitaka

Mundele kumfuata Ngoma Simba

Picha
Nimearifiwa kwamba nyota wa zamani wa AS Vita na Orlando Pirates Jean Makusu Mundele anatarajia kutua nchini siku ya Jumamosi pamoja na wakala wake Fausta World ili kukamilisha mazungumzo yake na klsbu ya Simba. Endapo kama watafikia makubaliano Mundele na asimba  watasaini mkataba wa miaka miwili ingawa pia mchezaji huyo anawindwa na Ihefu. Mundele ataungana na Fabrice Ngoma ambaye naye amewahi kucheza timu moja na Mundele, wawili hao walikuwa wanaichezea AS Vita  Mundele kujiunga na Simba

Kiungo mpya Simba akinukisha timu ya taifa Togo

Picha
Kiungo wa klabu ya Ihefu Sc Marouf Tchakei akiwa kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa ya Togo. Togo wanajiandaa na mechi mbili za kufuzu Kombe la dunia 2026 dhidi ya South Sudan (Juni 5) na DR CONGO (Juni 9) Kumbuka Simba Sc wako mbioni kuinasa Saini ya kiungo Huyo.

Mke wa Profesa Jay afunguka makubwa

Picha
Mke wake na Joseph Haule au Professor Jay wakati akiwa kwenye Interview na chombo kimoja cha TV amefunguka namna ambavyo walivyoweza kukutana na mume wake professor Jay kabla hawajawa wapenzi Ambapo kwa maelezo yake amesema kuwa yeye na Professor Jay walikutana American chips ya kinondoni ambapo alikuwa anaelekea field hivyo wakati huo ilikuwa asubuh alisimamishwa na baadae akaombwa namba ila alivyomuuliza jina akaambiwa anaitwa Joseph Lakini kuhusu kumpa namba alimpatia kwasababu wakati joseph anasimamishwa aliongeleshwa kwa heshima pia mbali na hivyo hakuwa anafahamu kama ni star mkubwa na maarufu lakini alikuwa anafikiri ni mpita kwasababu alikuwa si mpenzi wa mitandao

Yanga kumng' oa Chama kwa milioni 200

Picha
Klabu ya Yanga imempa ofa ya milioni 200 ya ada ya usajili na mshahara wa milioni 20 kwa mwezi kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia na klabu ya Simba SC, Clatous Chama ili asaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi.  Chama mwenye umri wa miaka 32 yupo tayari kusaini mkataba Yanga mara baada ya mkataba wake na Simba kuisha.

Joseph Guede hatihati kubaki Yanga

Picha
Mshambuliaji wa Yanga SC Joseph Guede amethibitisha kuwa mkataba wake na Yanga unamalizika Mwezi June mwaka huu lakini Hatma ya yeye kusalia kwenye Kikosi cha Yanga anamuachia Rais wa Yanga Engineer Hersi Said. Guede ambae alijiunga na Yanga wakati wa Dirisha dogo la usajili 2023/2024 alisaini kandarasi ya miezi sita ndani ya viunga vya Jangwani. Guede amethibitisha hayo wakati akifanya mahojiano na Crown Media wakati wa sherehe za Ubingwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Ligi inachezwa msimu huu, zawadi msimu ujao

Picha
Na Prince Hoza INASHANGAZA sana zawadi za washindi wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu wa 2023/2024 kupewa msimu ujao wa 2024/2025. Bodi ya Ligi pamoja Shirikisho la soka nchini, TFF limetangaza jana kwamba litatoa tuzo za washindi wa msimu huu wa Ligi Kuu bara. Bodi ya Ligi wamepanga kutoa tuzo hizo siku ya fainali ya Ngao ya Jamii msimu ujao, ikumbukwe Ngao ya Jamii ni ya kuashiria kuanza kwa msimu mpya. Malalamiko yamekuwa mengi juu ya maamuzi hayo ya kuwapa tuzo washindi wa msimu huu siku ya Ngao ya Jamii, wadau wanashangazwa sana uamuzi huo wakiamini TFF na Bodi ya Ligi haiwatendei haki wanaostahili kutunukiwa. Stephanie Aziz Ki mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara aliyepachika mabao 21 alistahili kupewa tuzo yake baada ya kumalizika ligi hiyo. Kumchelewesha sio sawa, ni uonevu juu yake, Aziz Ki ni raia wa Burkina Faso kwa vyovyote anarejea kwao hasa kwa sababu msimu umemalizika na mkataba wake na Yanga umeisha. Haijajulikana kama Aziz Ki ataendekea kuichezea Yanga, kwani zipo ...

Kinzumbi aitaka TP Mazembe imwachie akacheze Yanga

Picha
Winga wa klabu ya TP Mazembe, Philippe Kinzumbi ameuambia Uongozi wake wa TP Mazembe kuwa anahitaji kucheza soka katika ukanda wa Afrika Mashariki ( Tanzania ) kuelekea msimu ujao wa 2024/25. Licha ya TP Mazembe kumpa taarifa Philippe Kinzumbi kuwa vilabu vya Club Africain na MC Alger zimepeleka ofa rasmi kwa Kunguru wa Lubumbashi ili kupata huduma ya mchezaji huyo ambaye amekuwa na msimu bora sana lakini amekataa kwenda kucheza soka Uarabuni. Yanga itaendelea na mazungumzo na TP Mazembe mwanzoni mwa wiki ijayo ili kuipata saini ya Philippe Kinzumbi na inaamini kulingana na uhusiano wa baina ya vilabu hivi viwili basi watakuwa na wakati mzuri wa kumpata Kinzumbi ambaye amekubali kucheza Afrika Mashariki.

Diarra ashinda tuzo Afrika

Picha
Golikipa wa Klabu ya Yanga, Djigui Diarra ameshinda tuzo ya mchezaji bora Afrika msimu 2023/2024, tuzo hizi maalumu hutolewa nchini Mali kwa wachezaji wao waliofanya vizuri kwa msimu husika (Mali Football Awards). Diarra ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Sadio Kanoute kiungo mkabaji wa Simba, Fily Traore mshambuliaji wa TP Mazembe, Aliou Dieng kiungo mkabaji wa Al Ahly na Abdoulaye Kanou mshambuliaji wa USM Alger.

Kibu aigomea Taifa Stars

Picha
Winga wa Klabu ya Simba,Kibu Denis amegoma kujiunga na Kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya kambi iliyopo Indonesia kujiandaa na Mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Indonesia. Taarifa zinasema Kibu amesema anakwenda mapumziko nchini marekani.

Mo Dewji kuinunua Express ya Uganda

Picha
Mfadhili Wa Simba sc na Tajiri namba 17 barani Afrika Mohammed Dewji Yuko mbioni kununua Hisa asilimia 51% katika Klabu ya Express FC ya nchini Uganda. Baada ya kuwekeza katika Klabu za Tanzania sasa ni rasmi Mohamed amedhamiria kuwekeza Uganda. Express FC msimu huu imeshika nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi iyo ikiwa na jumla ya Alama 32 Ikiwa imefunga Magoli 36 na kuruhusu Magoli 38.

Taifa Stars ilivyoelekea Indonesia

Picha
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jana kimesafiri kuelekea nchini Indonesia kwa ajili ya mchezo wa kirafiki kujiandaa na mechi yake ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya timu ya taifa ya Zambia. Wachezaji wa timu hiyo wote waliungana pamoja na kukwea pipa kuelekea huko ambapo watacheza mchezo huo. Baadhi ya wachezaji hawakuonekana katika msafara huo akiwemo kiungo mshambuliaji wa Simba Kibu Denis

Simba na Azam zamgombea mshambuliaji wa San Pedro

Picha
Simba SC na Azam SC zote zimeulizia upatikanaji wa huduma ya mshambuliaji wa kati raia wa Ivory Coast ambaye kwa sasa anakipiga SAN PEDRO FC, Bedi Guy Stephanie (28). Mshambuliaji huyo mzoefu amekuwa katika kiwango kizuri tangu asajiliwe San Pedro kwani msimu huu ameshinda kiatu cha mfungaji bora akiwa na mabao 15. MCB MICHEZO, HERE WE GO 🤝👊🫵🛜💻

FAR Rabat yamtengea Inonga milioni 62 kwa mwezi

Picha
Taarifa kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika zinadai kuwa FAR Rabat ya nchini Morocco imemuandalia mshahara wa zaidi Tsh million 62 kwa mwezi mlinzi Henock Inonga Baka endapo atakubali kujiunga na miamba hiyo ya nchini Afrika Kaskazini. Tetesi zimekuwa zikamhusisha nyota huyo kujiunga na AS FAR Rabat na inaelezwa alishafikia makubaliano na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Morocco 'Botola Pro' toka Kipindi Cha michuano ya AFCON.

Winga Simba akoleza usajili wa Abdul Machela Coastal Union

Picha
Mchezaji wa zamani wa Simba SC Said Msasu amewaambia Coastal Union kwamba wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Black Bulls Lichinga ya Msumbiji Abdul Machela hawatakosea kwani anamjua dogo huyo ni moto wa kuotea mbali. Msasu ambaye aliwahi kuichezea Simba akitokea timu ya Friends Rangers ya Magomeni Kagera, anamjua vizuri Machela kwani aliwahi kumpeleka African Sports ya Tanga wakati yeye akiinoa Machela ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Simba SC, Ally Machela, anatajwa kujiunga na Coastal Union ya Tanga ambayo tayari ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu bara. Mbali na Coastal Union kumuwania Machela, Ihefu SC nayo inatajwa kumchukua kiungo huyo lakini pia timu yake ya Black Bulls imepanga kumuongeza mkataba ili kumbakisha Msasu aliandika yafuatayo: "Mmoja wa viungo bora kwa sasa namfuatilia sana tokea aende Msumbiji niliewahi kumpitisha kusajiliwa African Sports Said Msasu (kulia)...

Ley Matampi kinara wa clean sheet Ligi Kuu bara

Picha
Golikipa wa Coastal Union FC Ley Matampi (35) ndie ameibuka kuwa golikipa mwenye Clean Sheet nyingi msimu huu akiwa na Clean Sheat 15 mbele ya Djigui Diarra mwenye CleanSheet 14. Matampi ndiye kinara wa Clean Sheets ndani ya Ligi Kuu ya NBC akiwaacha Yona Amosi , Constantine Malimi , Djigui Diarra na John Noble na Jonathan Nahimana wakifuatia . Kumbuka Matampi ndiye Golikipa mwenye mafanikio zaidi ndani ya Ligi Kuu ya NBC akiwa ni mshindi wa CAF Champions League, CAF Confederation Cup bila kusahau ChAN 2016 akiwa na timu ya Taifa ya Congo DR

Tuzo za Ligi Kuu msimu huu kutolewa msimu ujao

Picha
Taarifa ya TFF iliyotolewa leo inasema hivi:- "Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sasa zitakuwa zikifanyika wakati wa michezo ya Ngao ya Jamil. Lengo la mabadiliko ya Hafla hizo za kuwatuza wachezaji bora wa msimu ni kufanya maboresho ya kulifanya tukio kuwa bora zaidi kukidhi malengo na mahitaji yake. Kwa mabadiliko hayo hafla ya Tuzo za TFF kwa msimu wa 2023/2024 itafanyika wakati wa michezo ya Ngao ya Jamii kufungua msimu wa 2024/2025. Tuzo za TFF ni tukio la kuzawadia wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano yanayoandaliwa na TFF/Bodi ya Ligi (TPLB) na matukio mengine rasmi yenye kuambatana na mpira wa miguu hapa chini. @hajismanara akaandika haya kwenye Insta yake:- "Viongozi wangu Wapendwa sana naogopa hata kuwashauri nisije kuonekane Bindeli, lakini haijawahi kutokea duniani kote tuzo za msimu huu zitolewe msimu ujao. Ngao ya Jamii ni mwanzo wa msim na mmeamua tuzo za msimu huu tulionao mzipeleke next season, mmetumia kigezo gani hasa Shirikisho...

John Bocco atundika daruga

Picha
John Bocco ametangaza kustaafu soka baada ya kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa zaidi ya Misimu 16. Bocco amefanikiwa kufunga magoli zaidi 100+ kwenye Ligi Kuu na kuwa Mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye historia ya Ligi Kuu. Mshambuliaji huyo aliyeibukia Cosmopolitan iliyokuwa inashiriki Ligi daraja la pili, alijiunga na Azam FC na alifanikiwa kuipandisha Ligi Kuu na pia kuipa ubingwa wa Ligi Kuu bara. Msimu wa 2017/2018 alijiunga na Simba na kuwapa mafanikio kadhaa na ameamua kustaafu na kujikita kwenye ukocha na sasa anafundisha timu ya vijana ya Simba B

Msimu ujao Yanga kuanzia hatua ya awali Ligi ya mabingwa Afrika

Picha
Kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika 24|25 klabu ya Yanga inaweza isianzie hatua ya awali | Preliminary round. Kwa mujibu wa (CAF) timu (10) za juu kwenye viwango wa (CAF) hazianzii preliminary round kwenye ligi ya Mabingwa. Currently club Ranking : 01. Al-Ahly Cairo (82) 02. Esperance de Tunis (61) 03. Wydad Casablanca (60) - ❌ 04. Mamelodi Sundowns (54) 05. Zamalek (43) - ❌ 06.RS Berkane (42) - ❌ 07. Simba SC (39) - ⚠️ 08. Petro Atletico - (39) 09. TP Mazembe - (38) 10. CR Belouizdad - (37) 11. USM Alger (36) - ❌ 12. Raja Casablanca - (35) 13. 🇹🇿 Young Africans SC - (31) 14. 🇨🇮 ASEC Mimosas - (30) 𝗞𝘄𝗮 𝗻𝗶𝗻𝗶 𝗮𝘀𝗶𝗮𝗻𝘇𝗶𝗲 𝗽𝗿𝗲𝗹𝗶𝗺𝗶𝗻𝗮𝗿𝘆 ? Klabu (4) zenye (X) zilizo juu ya Yanga SC kwenye viwango vya (CAF) hapo kwenye list hazitashiriki ligi ya Mabingwa Afrika 24|25, wanaenda Shirikisho (CAF). Maana yake ukizitoa timu hizo Yanga anaingia kwenye top (10) ya timu bora ambazo zina qualify kutoanzia hatua ya awali Preliminary round CAF champions league msimu u...

Aziz Ki aibuka mfungaji bora Ligi Kuu bara

Picha
Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC Stephanie Aziz Ki ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara inayodhaminiwa na NBC Bank. Aziz Ki amebahatika kufunga mabao 21 na kumzidi kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" aliyefunga mabao 18. Vita yao haikuwa rahisi kwani walishindana kwa mabao 18 mpaka inafika leo siku ya mwisho ambapo Aziz Ki akafunga mabao matatu (Hat trick) na kuchukua kiatu cha dhahabu. Hongera Aziz Ki kwa kuibuka mfungaji bora bila utata wowote

Alikiba aibomoa Wasafi FM

Picha
Mmiliki wa Crown FM Alikiba ameendelea kuzibomoa redio nyingine hasa baada ya leo kumnyakua mchambuzi wa Wasafi FM Hans Rafael. Alikiba mapema leo ameposti katika ukurasa wake akimtambulisha mchambuzi huyo ambaye pia amedai ni shabiki yake Alikiba ameandika kuwa "HANS! @hansrafael14 Mimi ni miongoni mwa Mashabiki wa kazi yako, namna unavyochambua Football na kuufanya uonekane mchezo wa kimahesabu unanikumbusha enzi zangu wakati nakipiga pale Coastal Union. Nilikuwa mtu Mnyama sana Leo nina furaha Sana, nakuwa zaidi ya shabiki yako baada ya kuungana na kufika Nyumbani CROWN MEDIA. Karibu tuwahudumie na kuwapa furaha Wapenda Michezo. Karibu sana MTAALAM y @hansrafael14 Kwenye Chama la KIMKAKATI 92.1 @crownfmtz! Aliandika Alikiba

Ligi Kuu bara yamalizika kibabe

Picha
Ligi Kuu Tanzania bara imemalizika rasmi leo hii na Yanga SC ikiibuka mabingwa wakati Mtibwa Sugar na Geita Gold zikishuka daraja. Azam FC imeshika nafasi ya pili wakati Simba SC wakishika nafasi ya tatu na Coastal Union ikishika nafasi ya nne hivyo sasa zimepata nafasi ya kuwakilisha nchi katika michuano ya CAF. Yanga SC imeifunga Tanzania Prisons mabao 4-1, wakati Simba SC ikiifunga JKT Tanzania mabao 2-0, Azam F. iki heza ugenini imeifunga Geita Gold mabao 2--0 na Coastal Union ikienda sare 0-0 na KMC. Matokeo mengine ni kama ifuatavyo, Ihefu SC 2- Mtibwa 0, Mashujaa 3 Dodoma Jiji 0, Namungo 3 Tabora United 2, Singida Fountain Gate 2 Kagera Sugar 3,

Azam FC yashusha Mcolombia mwingine

Picha
Mshambuliaji Jhonier Blanco (23) anakaribia kuwa mchezaji mpya wa Azam fc timu ya Tanzania. Kuna makubaliano ya pande mbili kati ya Azam fc na klabu ya Águilas Doradas. Mshambulizi huyo atasafiri saa chache zijazo ndani ya wiki hii anaweza kutambulishwa na klabu ya Azam fc. Katika klabu ya Azam fc kuna Wakolombia wawili: Franklin Navarro na Yeison Fuentes

Simba yatua kwa Mzize

Picha
Klabu ya Simba imeonyesha nia ya kutaka kumsajili straika wa Yanga, Clement Mzize ambaye amekuwa na msimu bora Jangwani. Simba baada ya kuona upo uhitaji wa straika ili kuimarisha kikosi chao, klabu hiyo moja kwa moja imemlenga Mzize na sasa viongozi wamelivalia njuga suala hilo.

Aziz Ki atasaini Yanga- Mobeto

Picha
Na Ikram Khamees Mwanamitindo na msanii wa bongo muvi Hamisa Mobeto amesema mchezaji wa Stephanie Aziz Ki atahakikisha anabaki katika klabu ya Yanga. Mobeto ameyasema hayo juzi kwamba atahakikisha kinara huyo wa mabao anasaini tena Yanga na akiendelea kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo. Mobeto ambaye aliwahi kuonekana kwenye klabu ya Simba, akiwa kama shabiki wake, lakini ameonekana Yanga. Msanii huyo mrembo zaidi hapa nchini ameonekana kumdatisha staa huyo wa Yanga, Aziz Ki anataka kuondoka kwenye kikosi hicho na inadaiwa anaweza kujiunga na timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika au Pyramids ya Misri Hamisa Mobeto

Ranga Chivaviro atoka kapa

Picha
Wachezaji wawili waliosajiliwa katika dirisha moja msimu uliopita wakitokea katika klabu moja ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini iliyoshika daraja, wametwaa Ubingwa Wakati klabu ya Marumo Gallants ikishuka daraja katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini kuna nyota wake 3 walionekana kuwa lulu sokoni na kupata timu kwa haraka zaidi Skudu aliamua kwenda Yanga SC ya Tanzania na Lesiba nae akaenda zake Mamelodi Sundowns ya hapo hapo kwao Afrika Kusini, Siku ya jana usiku Mamelodi Sundowns wamekabidhiwa kombe lao la Ligi Kuu licha ya kupokea kichapo cha 0-1 dhidi ya Capetown City ambao wameikatisha UNBEATEN run ya Mamelodi Sundowns Ligi kyuu iliyodumu msimu nzima katika mechi ya mwisho kwa Msimu huu, Huku pia usiku pia Young Africans SC walikabidhiwa kombe lao la Ligi Kuu baada ya kushinda 3-0 dhidi ya Tabora United. Wakati Ranga Chivaviro yeye alielekea zake Kaizer Chiefs ambako mpaka msimu huu unatamatika hajainua makwapa

SIRI ZA AZIZ KI KUIBA UCHAWI WA PACOME ZAVUJA

Picha
Na Mwandishi Wetu Kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz Ki raia wa Burkina Faso ni kama amechukua uchawi wa kiungo mwenzake Pacome Zouzoua raia wa Ivory Coast. Pacome kabla hajaumia alikuwa mchezaji kipenzi cha Wanayanga na alikuwa akicheza kwa umahiri wa hali ya juu, Aziz Ki na umahiri wake wa kupiga mashuti makali bado alikuwa hamfikii Pacome. Pacome ana mtindo wake wa kupaka rangi nyeupe nywele zake na zilimpatia umaarufu mkubwa, kuna wakati nywele hizo za rangi nyeupe zilionekana kama uchawi wake ndani ya uwanja. Aziz Ki alianza kupaka rangi nyeupe wakati Yanga ilipompa Pacome mechi yake moja iliyoitwa Pacome Day ambapo Yanga ilicheza na CR Belouizdad ambapo Yanga ilishinda mabao 4-0. Kuanzia hapo Aziz Ki hakuacha kupaka rangi na akaendelea hivyo mpaka sasa, nyota ya Aziz Ki ikawa juu huku ya Pacome ikazima, kwasasa Aziz Ki anapendwa zaidi kwenye kikosi cha Yanga wakati Pacome anaonekana wa kawaida Aziz Ki Pacome

ABDUL MACHELA AZIINGIZA VITANI COASTAL, IHEFU

Picha
Vilabu vya Coastal Union ya Tanga na Singida Black Stars (Ihefu) ya Singida vimeingia vitani kutaka kuiwania saini ya mchezaji wa klabu ya Black Bulls ya Msumbiji Abdul Machela raia wa. Tanzania. Zaandani kabisa kutoka kwa mwanahabari wetu zinasema Mtanzania huyo anayeichezea timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza nchini humo anahitajika kwa udi na uvumba na huenda msimu ujao atakuwemo kwenye Ligi Kuu bara. Machela anayecheza nafasi ya ushambuliaji anatajwa kusajiliwa na Coastal Union ya Tanga ambayo imevutiwa naye, lakini Singida Black Stars nayo inataka kuwazidi kete Wanamangushi hao wa Tanga. Ikumbukwe Coastal Union msimu ujao itashiriki kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kumaliza kwenye nafasi ya nne Ligi Kuu bara Abdul Machela anatakiwa na timu mbili za Coastal na Ihefu

Straika Nigeria aambiwa watoto wake sio damu yake

Picha
Imebainika kuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria Kayode Olarenwaju watoto watatu ambao ilisemekana ni wake yeye na mke wake,kipimo Cha DNA kimethibitisha kuwa sio watoto wake wote hao wala hawaendani kwa damu. Kwa mujibu wa taarifa za mfanano ni kuwa watoto hao wanaelezwa kuwa wa Pastor mmoja mkubwa nchini Nigeria ambae jina lake hakijawekwa wazi. Olarenwaju alibambikwa watoto hao.

Al Ahly na ubingwa wa 12 Ligi ya mabingwa Afrika

Picha
Klabu ya Al Ahly ya Misri imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya 12 kufuatia ushindi wa jumla wa 1-0 dhidi ya Esperance ya Tunisia. Bao pekee la kujifunga la Roger Aholou dakika ya 4 limetosha kuwapa ubingwa Ahly. Mchezo wa fainali ya kwanza iliyopigwa Tunisia ulimalizika kwa sare tasa kabla ya Al Ahly kutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kushinda 1-0 nyumbani. Al Ahly wanatwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita

Moroko amtosa Job Stars

Picha
Kaimu kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars Hemed Moroko ameendelea kutomjumuhisha beki wa kati wa Yanga SC Dickson Job kwenye kikosi chake baada ya leo kutangaza kikosi kitakachojiandaa kucheza Zambia, Chipolopolo. Kocha huyo ameweka mkazo wa kutomuita Job hass baada ya kumkatalia kucheza namba mbili kama alivyowahi kusema wakati alipokuwa anajibu maswali ya wanahabari juu ya kutomuita beki huyo kipenzi cha Wanayanga. Katika kikosi alichoita leo, Moroko amewataja baadhi ya nyota ambao watakuwemo kwenye kikosi cha awali

Simba yakubali yaishe kwa Chama, kumlipa dau anslotaka

Picha
Klabu ya Simba imekubali kuboresha zaidi mkataba kwa matakwa mbalimbali anayohitaji kiungo raia wa Zambia, Clatous Chama ili asaini mkataba mpya, Clatous Chama yupo tayari kusaini kandarasi mpya na kipaumbele kikubwa zaidi ni Simba, kuelekea msimu ujao,

Aziz Ki ataendelea kucheza Yanga misimu miwili ijayo

Picha
Hatimaye kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa Tanzania bara mara 30 Yanga SC, Stephanie Aziz Ki amewahakikishia mashabiki wa klabu hiyo waliojitokeza kwenye paredi la maadhimisho ya kusherehekea ubingwa leo makao makuu Jangwani kwamba ataendelea kusalia kikosini misimu miwili ijayo. Hayo yote yametokana na msanii Harmonize ambaye aliambatana naye stejini na kumuomba awaambie mashabiki wa timu hiyo hatma yake baada ya kusikia tetesi kwamba anataka kuondoka. Aziz Ki kwa mdomo wake amesema hawezi kuondoka Yanga na ataendelea kwa misimu miwili ijayo, naye Rais wa klabu hiyo Injinia Said amedai Aziz Ki hawezi kuondoka mpaka pale Yanga itakapotimiza malengo yao

Azam FC yaanza na Meza wa Colombia

Picha
Azam FC imemtambulisha, Ever Meza, kama kiungo wao mpya aliyenunuliwa kutoka klabu ya Leonnes ya Colombia. Meza, raia wa Colombia aliyezaliwa Julai 21, 2000; alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Alianza FC ya huko huko Colombia. Amesaini mkataba wa miaka minne utakaomuweka Azam Complex hadi mwaka 2028. Karibu sana Ever William Meza Mercado

Katwila asimamishwa Mtibwa Sugar

Picha
Na Salum Fikiri Jr Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar Umefikia maamuzi ya kumsimamisha kazi kocha wake mkuu Zuberi Katwila na benchi lake wakiwapo Kocha wa Makipa Patrick Mwangata na Meneja wa timu Henry Joseph, Huku pia CEO wa klabu hiyo Abraham Josh nae akiendelea kuwa nje ya klabu hiyo kutokana na Mwenendo mbaya wa timu, Kwasasa kikosi kitaendelea kuwa Chini ya Kocha Msaidizi Awadh Juma 'Maniche', Kwasasa Mtibwa Sugar ipo chini ya msimamo ikiwa na alama 21, baada ya michezo 28, huku siku ya Kesho ikishuka dimbani katika Uwanja wa ugenini kumenyana na Mashujaa FC, Mtibwa Sugar watamaliza Msimu wao kwa kumenyana na Ihefu FC ambayo itakuwa mechi yao ya kufungia msimu wa 23/24.

Feitoto jino kwa jino na Aziz Ki

Picha
Kiungo Feisal Salum amefunga mabao mawili kwenye ushindi wa 5-1 walioupata Azam FC mbele ya Kagera Sugar kwenye muendelezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara Mabao hayo yamemfanya nyota huyo kufikisha mabao 18 kwenye vita vya kuwania kiatu cha dhahabu dhidi ya kiungo nyota wa Yanga SC Stephane Aziz Ki aliyepachika bao moja kwenye ushindi wa 3-0 walioupata mabingwa wa ligi hiyo mbele ya Tabora United. Bao hilo limemfanya nyota huyo kufikisha mabao 18 sawa na nyota huyo wa Azam FC. Sasa hatma ya vita hivyo itaenda kumalizwa kwenye michezo ya mwisho kabisa ya ligi kuu ambapo Azam FC watakuwa ugenini mbele ya Geita Gold wakati Yanga SC watakamilisha ratiba dhidi ya Tanzania Prisons Azam FC sasa imebakiza ushindi mmoja tu kujihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao na kumaliza juu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Man United mabingwa FA

Picha
Manchester United imeifunga Manchester City na kufanikiwa kubeba ubingwa wa Kombe la FA 2024, kwa kuitandika goli 2-1 kwenye Uwanja wa Emirates Jijini London na kufanya United kubeba kombe hilo kwa mara 13 ambapo mara ya mwisho kulibeba kombe hilo ilikuwa Mwaka 2016. Kutakata kwa Manchester United kumetokana na magoli ya Alejandro Garnacho pamoja na Kobbie Mainoo, huku kwa Manchester City ikiwa imepata goli kupitia kwa Jeremy Doku. ⚽️ 30" Garnacho ⚽️ 39" Mainoo ⚽️ 87" Doku

FIFA yawaalika makocha wa Afrika kwenye droo ya kombe la dunia

Picha
FIFA wame waalika makocha Wakuu baadhi Kutoka Bara la Afrika kuhuduria Draw ya Kombe la Dunia Ngazi ya Klabu makocha hao ni kutokea katika vilabu Vifuatazo. 🔹 Al Ahly🇪🇬 🔹 ES Tunis🇹🇷 🔹 Mamelodi Sundowns🇿🇦 🔹Wydad 🇲🇦 Mbali na makocha hao wame jumuishwa pia viongozi wawili kuhuduria Draw iyo itakayo fanyika Marekani mwenzi ujao. Lakini pia watafanikiwa kutembelea viwanja mbali mbali vitakavyo tumika katika Michuano iyo. Kumbuka kombe la Dunia ngazi ya Klabu litafanyika 2025.

Saido moto wa kuotea mbali, Simba ikishinda kiducuu

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo imeifunga timu ya KMC ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kuilaza bao 1-0 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha mchezo wa Ligi Kuu bara. Licha ya ushindi huo Simba bado inaendelea kushika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 ikizidiwa na magoli ya kufunga na Azam ambayo leo imeichapa Kagera Sugar mabao 5-1 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi. Goli pekee la Simba lilifungwa dakika ya 2 na Said Ntibanzokiza "Saido", mechi nyingine zilizochezwa leo ni Yanga 3 Tabora United 0 Azam 5 Kagera Sugar 1 Mashujaa 3 Mtibwa Sugar 2 Ihefu 0 Dodoma Jiji 1 Singida FG 2 Geita Gold 1 Namungo 2 Prisons 2 Coastal Union 0 JKT Tanzania 0