Kinzumbi aitaka TP Mazembe imwachie akacheze Yanga


Winga wa klabu ya TP Mazembe, Philippe Kinzumbi ameuambia Uongozi wake wa TP Mazembe kuwa anahitaji kucheza soka katika ukanda wa Afrika Mashariki ( Tanzania ) kuelekea msimu ujao wa 2024/25.

Licha ya TP Mazembe kumpa taarifa Philippe Kinzumbi kuwa vilabu vya Club Africain na MC Alger zimepeleka ofa rasmi kwa Kunguru wa Lubumbashi ili kupata huduma ya mchezaji huyo ambaye amekuwa na msimu bora sana lakini amekataa kwenda kucheza soka Uarabuni.

Yanga itaendelea na mazungumzo na TP Mazembe mwanzoni mwa wiki ijayo ili kuipata saini ya Philippe Kinzumbi na inaamini kulingana na uhusiano wa baina ya vilabu hivi viwili basi watakuwa na wakati mzuri wa kumpata Kinzumbi ambaye amekubali kucheza Afrika Mashariki.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA