Feitoto jino kwa jino na Aziz Ki
Kiungo Feisal Salum amefunga mabao mawili kwenye ushindi wa 5-1 walioupata Azam FC mbele ya Kagera Sugar kwenye muendelezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara
Mabao hayo yamemfanya nyota huyo kufikisha mabao 18 kwenye vita vya kuwania kiatu cha dhahabu dhidi ya kiungo nyota wa Yanga SC Stephane Aziz Ki aliyepachika bao moja kwenye ushindi wa 3-0 walioupata mabingwa wa ligi hiyo mbele ya Tabora United. Bao hilo limemfanya nyota huyo kufikisha mabao 18 sawa na nyota huyo wa Azam FC.
Sasa hatma ya vita hivyo itaenda kumalizwa kwenye michezo ya mwisho kabisa ya ligi kuu ambapo Azam FC watakuwa ugenini mbele ya Geita Gold wakati Yanga SC watakamilisha ratiba dhidi ya Tanzania Prisons
Azam FC sasa imebakiza ushindi mmoja tu kujihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao na kumaliza juu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC kwenye msimamo wa Ligi Kuu.