Katwila asimamishwa Mtibwa Sugar

Na Salum Fikiri Jr

Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar Umefikia maamuzi ya kumsimamisha kazi kocha wake mkuu Zuberi Katwila na benchi lake wakiwapo Kocha wa Makipa Patrick Mwangata na Meneja wa timu Henry Joseph,

Huku pia CEO wa klabu hiyo Abraham Josh nae akiendelea kuwa nje ya klabu hiyo kutokana na Mwenendo mbaya wa timu,

Kwasasa kikosi kitaendelea kuwa Chini ya Kocha Msaidizi Awadh Juma 'Maniche',

Kwasasa Mtibwa Sugar ipo chini ya msimamo ikiwa na alama 21, baada ya michezo 28, huku siku ya Kesho ikishuka dimbani katika Uwanja wa ugenini kumenyana na Mashujaa FC,

Mtibwa Sugar watamaliza Msimu wao kwa kumenyana na Ihefu FC ambayo itakuwa mechi yao ya kufungia msimu wa 23/24.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA