ABDUL MACHELA AZIINGIZA VITANI COASTAL, IHEFU
Vilabu vya Coastal Union ya Tanga na Singida Black Stars (Ihefu) ya Singida vimeingia vitani kutaka kuiwania saini ya mchezaji wa klabu ya Black Bulls ya Msumbiji Abdul Machela raia wa. Tanzania.
Zaandani kabisa kutoka kwa mwanahabari wetu zinasema Mtanzania huyo anayeichezea timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza nchini humo anahitajika kwa udi na uvumba na huenda msimu ujao atakuwemo kwenye Ligi Kuu bara.
Machela anayecheza nafasi ya ushambuliaji anatajwa kusajiliwa na Coastal Union ya Tanga ambayo imevutiwa naye, lakini Singida Black Stars nayo inataka kuwazidi kete Wanamangushi hao wa Tanga.
Ikumbukwe Coastal Union msimu ujao itashiriki kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kumaliza kwenye nafasi ya nne Ligi Kuu bara