Aziz Ki ataendelea kucheza Yanga misimu miwili ijayo

Hatimaye kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa Tanzania bara mara 30 Yanga SC, Stephanie Aziz Ki amewahakikishia mashabiki wa klabu hiyo waliojitokeza kwenye paredi la maadhimisho ya kusherehekea ubingwa leo makao makuu Jangwani kwamba ataendelea kusalia kikosini misimu miwili ijayo.

Hayo yote yametokana na msanii Harmonize ambaye aliambatana naye stejini na kumuomba awaambie mashabiki wa timu hiyo hatma yake baada ya kusikia tetesi kwamba anataka kuondoka.

Aziz Ki kwa mdomo wake amesema hawezi kuondoka Yanga na ataendelea kwa misimu miwili ijayo, naye Rais wa klabu hiyo Injinia Said amedai Aziz Ki hawezi kuondoka mpaka pale Yanga itakapotimiza malengo yao


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA