Ranga Chivaviro atoka kapa
Wachezaji wawili waliosajiliwa katika dirisha moja msimu uliopita wakitokea katika klabu moja ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini iliyoshika daraja, wametwaa Ubingwa
Wakati klabu ya Marumo Gallants ikishuka daraja katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini kuna nyota wake 3 walionekana kuwa lulu sokoni na kupata timu kwa haraka zaidi
Skudu aliamua kwenda Yanga SC ya Tanzania na Lesiba nae akaenda zake Mamelodi Sundowns ya hapo hapo kwao Afrika Kusini,
Siku ya jana usiku Mamelodi Sundowns wamekabidhiwa kombe lao la Ligi Kuu licha ya kupokea kichapo cha 0-1 dhidi ya Capetown City ambao wameikatisha UNBEATEN run ya Mamelodi Sundowns Ligi kyuu iliyodumu msimu nzima katika mechi ya mwisho kwa Msimu huu,
Huku pia usiku pia Young Africans SC walikabidhiwa kombe lao la Ligi Kuu baada ya kushinda 3-0 dhidi ya Tabora United.
Wakati Ranga Chivaviro yeye alielekea zake Kaizer Chiefs ambako mpaka msimu huu unatamatika hajainua makwapa