Kelvin John ajiunga timu ya Ligi Kuu Denmark
Mshambuliajia wa Taifa Stars anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji Kelvin John (20) amesaini Mkataba wa miaka minne kuichezea Klabu ya Aalborg FC iliyopanda daraja na sasa itacheza Ligi Kuu ya Denmark msimu wa 2024/2025.
Kelvin alijiunga na KRC Genk 2021 na baadae kupandishwa timu ya wakubwa 2022 ila hakupata nafasi sana ya kucheza.