Simba yatua kwa Mzize
Klabu ya Simba imeonyesha nia ya kutaka kumsajili straika wa Yanga, Clement Mzize ambaye amekuwa na msimu bora Jangwani.
Simba baada ya kuona upo uhitaji wa straika ili kuimarisha kikosi chao, klabu hiyo moja kwa moja imemlenga Mzize na sasa viongozi wamelivalia njuga suala hilo.