Alikiba aibomoa Wasafi FM
Mmiliki wa Crown FM Alikiba ameendelea kuzibomoa redio nyingine hasa baada ya leo kumnyakua mchambuzi wa Wasafi FM Hans Rafael.
Alikiba mapema leo ameposti katika ukurasa wake akimtambulisha mchambuzi huyo ambaye pia amedai ni shabiki yake
Alikiba ameandika kuwa "HANS! @hansrafael14 Mimi ni miongoni mwa Mashabiki wa kazi yako, namna unavyochambua Football na kuufanya uonekane mchezo wa kimahesabu
unanikumbusha enzi zangu wakati nakipiga pale Coastal Union.
Nilikuwa mtu Mnyama sana
Leo nina furaha Sana, nakuwa zaidi ya shabiki yako baada ya kuungana na kufika Nyumbani CROWN MEDIA.
Karibu tuwahudumie na kuwapa furaha Wapenda Michezo.
Karibu sana MTAALAM y @hansrafael14 Kwenye Chama la KIMKAKATI 92.1 @crownfmtz! Aliandika Alikiba