Aziz Ki aibuka mfungaji bora Ligi Kuu bara

Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC Stephanie Aziz Ki ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara inayodhaminiwa na NBC Bank.

Aziz Ki amebahatika kufunga mabao 21 na kumzidi kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" aliyefunga mabao 18.

Vita yao haikuwa rahisi kwani walishindana kwa mabao 18 mpaka inafika leo siku ya mwisho ambapo Aziz Ki akafunga mabao matatu (Hat trick) na kuchukua kiatu cha dhahabu.

Hongera Aziz Ki kwa kuibuka mfungaji bora bila utata wowote


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA